Mlimbwende Gabriela Isler, ambaye ni Miss Universe Venezuela 2013, anavishwa taji na  Olivia Culpo, Miss Universe 2012, kwenye fainali za Miss Universe katika ukumbi wa  Crocus City Hall jijini Moscow, Russia, usiku wa kuamkia leo. Kwa ushindi huo Venezuelan imeshashinda mataji 7 ya Miss Universe, 6 ya Miss World, 6 Miss International na 1 la Miss Earth. 
 Bongo bado tupo tupo kwanza, ingawa mwakilishi wetu Betty Boniface kajitahidi sana kwa mavazi ya nyumbani na pozi za kimataifa kama inavyoonesha hapo chini. Iko siku na sisi tutakenua tu...
 Betty alitinga na mavazi ya Tingatinga mkeka wa ukindu na 
Vazi la Batik na urembo wa Kimasai vilimtoa vilivyo. Ila basi tu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Siyo basi tu, RANGI YA MIILI YENU, NDO NOMA.

    ReplyDelete
  2. naungana na wewe mdau, ukiangalia wale wasichana karibu wote si lugha ni rangi, akipewa mweusi nafasi ya 16 au ya 10 ni kufunika maboya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...