Awali ya yote Hospitali ya Taifa Muhimbili inapenda kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wa Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki katika Hospitali ya Millpark, Johanesburg nchini Afrika Kusini.  Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi, roho ya marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Amina.

Katika gazeti la Rai Nguvu ya Hoja Toleo Na. 1092 la Jumatano Novemba 20, 2013 lilichapisha habari ukurasa wa tatu ikisomeka “Maisha ya Dkt. Mvungi yangewezwa kuokolewa”

Gazeti hilo lilidai kwamba baada ya marehemu Dkt. Mvungi kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ilichukua zaidi ya saa sita kabla ya kupatiwa  huduma ya dharura aliyokuwa akihitaji na kwamba ni jambo la kawaida katika Hospitali hii ya Taifa.

Tunapenda kuwafahamisha umma wa Tanzania kuwa Idara ya  Huduma za Dharura ya Hospitali ya Taifa (EMD) imeimarika sana na huchukua takribani kati ya dakika 30-45 tu kwa  mgonjwa wa ajali kuhudumiwa na kupelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa matibabu zaidi. Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Marehemu Dr. Sengondo Mvungi.

Tunaomba radhi kwa huduma ya kwanza ya CT Scan kutofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na tatizo lililosababishwa na mawasiliano. Hata hivyo, huduma ya CT Scan ya mara ya pili ilifanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na ilisaidia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha tiba aliyokuwa anapatiwa na madaktari wa MOI.

Tunaendelea kusisitiza kuwa uandishi wa habari za afya unahitaji kuzingatia maadili ya sekta ya afya ili kutosababisha usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.

Ni matumaini yetu kuwa Waandishi wa Habari watazingatia maadili ya kazi zao kama tunavyoshauri mara kwa mara katika matoleo yanayohusu Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Imetolewa na;

Ofisi ya Uhusiano
Hospitali ya Taifa Muhimbili
Novemba 22, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. DAKIKA 30 MPAKA 45 MTU AMEPATA AJALI AMESHAVUJA SANA,NI RAHISI KUPOTEZA MAISHA.TUBADILIKE JAMANI,AGALAO UNGESEMA DAKIKA 15.MDAU LONDON.

    ReplyDelete
  2. Duh ... Jamani huduma ya A&E huchukua dk 30 mpk 45 kwa mgonjwa kupatiwa huduma??? eti hapo ndiyo wame-improve mnacheza na maisha ya watu nyie... kwa hili RAI wako right !!

    ReplyDelete
  3. Hakuna tiba ya maana hapo cha muhimu Mudy peleka mgojwa wako hospital binafsi tutakwesha.

    ReplyDelete
  4. Emergency Medicine specialists wanaita kitu GOLDEN HOUR,bila shaka mtaalam huyu wa Muhimbili amesahau kuwa chances of survival and prevention of death decreases after that. Jee huyu mgonjwa alichukua muda gani kabla ya kupata matatibabu.Kisha hataki kutueleza hayo matatizo ya mawasiliano yalisababisha kuchelewa kwa mhuduma kwa muda gani, na ni matatizo gani yakuzuia mtu aliyepigwa panga kichwani kusaidiwa.

    ReplyDelete
  5. Huyu alie justify kilichotokea..... ningemuomba atazame series ya kitambo kidogo ambayo bado inarushwa hewani toka USA.....iitwayo ER(EMERGENCY ROOM)na hizo dakika 30-45 zako.

    ReplyDelete
  6. This is laughable to say the least. Did u read the lame excuses by Prof Museru refuting findings by the South Asfrican doctors that treated the late Prof Mvungi concerning the late diagnosis of pressure exerted on the brain as a cause of death? One characteristic of a distinguished establishment is to admit errors when they occur and seek to remedy them. Muhimbili is way too far from becoming one.

    ReplyDelete
  7. Huduma ya kwanza ya CT Scan kutofanyika Muhimbili ndio tatizo kubwa ambalo linalalamikiwa na gazeti pamoja na umma wa watanzania. Hatutaki kujua ni kwa kiwango gani mmeimarika kama mnashindwa kuzuia majanga kama haya. Kila roho ipoteayo ina haki ya kutetewa pasipo kuangalia roho zingine zilizopona. Kupotea kwa Dr. Mvungi hakuwezi kujadiliwa na takwimu za maendeleo mnayoyasema ya dk 30-45 za wagonjwa wa dharura.

    Ni tatizo kama hilo ndilo linalotokea kwa wagonjwa walio wengi, halafu hospitali inaishia kuomba radhi kwa kusema eti 'tatizo limesababishwa na mawasiliano'. We cannot accept such a lousy excuse from Muhimbili.

    Katika hili, sikutegemea kama Muhimbili mngegeuka wanasiasa badala ya wanataaluma.

    ReplyDelete
  8. Constructive criticism is good for Muhimbili, pick up the good and improve service delivery.

    ReplyDelete
  9. Binafsi sishangazwi na taarifa za gazeti la Rai kwani siku hizi limeshapoteza kabisa ile credibility waliyokuwa nayo ya umakini wa kutoa taarifa. Wamekuwa ni wabunifu wakubwa wa habari na wanatia kichefuchefu.

    ReplyDelete
  10. Liwepo deski maalum la KIPOLISI ktk kila hospitali kubwa ya wilaya, mkoa na rufani ili kunapotokea majeruhi wakimbizwe moja kwa moja hospitali badala ya kupitia KITUO cha POLISI kupata fomu ya PF3.

    Deski maalum la KIPOLISI ktk hospitali tajwa hapo mwanzo litashugulikia kutoa fomu ya PF 3 huku majeruhi wakipatiwa huduma za kuokoa maisha yao ndani ya hospitali.

    Na Pia Deski hilo maalum la KIPOLISI hospitalini litawasiliana na jeshi la POLISI kuhusu dhahama iliyompata majeruhi iwe ukatili wa kijinsia, ajali, kupigwa na wananchi wenye harisa kali au kushambuliwa na vitu vya ncha kali n.k

    Kwa utaratibu huo hapo juu HOSPITALI zitaweza kunusuru maisha ya majeruhi wengi kwa kutoa huduma ndani ya dakika 45 baada ya tukio.

    Mdau
    Makini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...