![]() |
Said A. Arfi (MB) |
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako (Mwenyekiti Taifa CHADEMA) taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.
Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu. Pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.
Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi.Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu
Nawasilisha.Said A. Arfi (MB)
hoja zako zimetulia endelea kuwa na msimamo wa kusimamia haki unapoina bila kuterereka na endelea kupinga lile lisilokuwa na manufaa kwa jamii bila ya kutetereka. kila la kheri katika kutumikia taifa na Muumba akusaidie na uwe na mwisho mwema
ReplyDeleteKAKA WE KAA PEMBENI SIFA ZA CHADEMA HUNA KWANZA SIO MCHAGA AU KASKAZIN PIL SIO MKRISTO HAI AU MARANGU MKAKATI CDM NI KUBAKI WAO TU. WA KASKAZIN JAMAN MBOWE KANUNUA NYUMBA DUBAI KWA CASH MONEY HAKUNA MTU ANAYEOJI KAJIPA TENDA MWENYEWE YA KUNUNUA MAGARI, PIKIPIKI NA RUKZUKU ANATUMIA MWENYEWE NA BABA MKWE WAKE MTEI MBONA HAMUULIZI HIVI KATIBA YA CHAMA KUBADILSHWA NI YA ZITO AU HAMUONI UPUUZI HUU WA MBOWE WACTH OUT CHAMA KIZURI ILA MBOWE NA MTEI WANA TAMAAA SANA NA MADARAKA
ReplyDeleteGOOD! you better exit before we suck you out, we have long list of capable guys here to man your position much better than you did.
ReplyDeleteNi heri;na ungeeleweka zaidi,kama ungejiuzulu kabisaaaa!!!!!!!!!! hata huo uanachama ili ujiondoe kwenye hayo"matatizo"ambayo umeyabaini nafsini mwako.Mtu wa cheo chako katika chama hafai kujihisi hili au lile bila ya kuhoji kulikoni wala kukosoa mtindo wa "kuchaguliwa Viongozi na Muasisi".Naelewa ubunge wako unalindwa na mbinu mpya ya kisiasa
ReplyDeleteiliyobuniwa ili muasi toka vyama vya upinzani kwa ulaini. Ila itakuwaje ktk uchaguzi 2015?
Nathani wewe ndie mnafiki wa kwanza.Kama uliyo hayo mwanzoni kwani ni hukuhoji na kutafutia ufumbuzi.Swala la dini lisiwatenge watanzania leta hoja za msingi.
ReplyDeletenachoona kwangu kisa Zitto Kabwe kwenda nawewe unaona ni sawa sababu ni muislam mwenzangu.Simamia hoja.
Tatu,hii sio hoja ya wewe kujiuzulu.Kwa taarifa yako Zitto alishapata kusikia mengi na kusemwa na mengi lakni aliendelea kukaa ndani ya chadema mpaka hapo mwishoni walipomsimamisha.Nasubiri kuona nini Zitto atakuja nalo.Lakni kwa hili la kwako ni la kipuuzi.
Mhe. Arfi karibu CCM !
ReplyDeleteAchana na Chama chenye Siasa za Ukoo na Ukabila.
Huelewi ndugu?, hapo wanataka mpungue ili wao kwa wao wapitishane ktk Kiti cha Mgombea Uraisi!
Hiyo yote ni pangua pangua ya Gombania Goli kuelekea 2015.
Undeni chama chenu, hicho ni cha watu wa kaskazini nyinyi mulidandia bila kujuwa.
ReplyDeleteWewe mdau uliyeanza na neno "Nathani"ambalo pia umelikosea, hakuna sehemu ambayo Arfi ametoa sababu za kidini. Hiyo ni tafsiri yako mwenyewe kutoka katika ubongo wako uliojaa udini.
ReplyDeleteAmezungumzia uhusiano wake yeye na Pinda, kwani Pinda tangu lini amekuwa muislamu? Au yeye alichaguliwa na waislamu watupu?
Jaribuni kujibu hoja zake na sio kuingiza mambo ya kidini ambayo hayana maana yo yote.
Acheni uhananga wenu hao chadema wanaendeleza ukaskazini wao wengeachiwa chama chao cha ubaguzi mana haingii akili wote wenye nyadhifa za juu watoke huko kaskazini wana mambo ya kibaguzi mwanangu nyepesi waachie chama chao cha udini hao washaona kimepata umaarufu sasa kwa ajili ya vijana wanaleta ujinga wao
ReplyDeleteCongrats CHEDEMA get rid of all those hangers on and then complete the transformation and change the name from CHEDEMA to CHAWACHAGA
ReplyDeleteKwa hiyo waisilamu wote ndani ya CDM wanaamua kumfuata Zitto kabwe muisilamu mwenzao? Ndio maana Baregu naye kajiuzulu. Sawa tu Yote ni sawa tu.
ReplyDeleteWENGI HUTOA MAONI MAZURI, ILA WENGINE WANA MAWAWO FINYU, HIVYO WAACHE WATOE UPUPU WAO au ZISITOLEWE KABISA COMMENTS ZAO
ReplyDeleteWewe uliyeanza na 'Nathani' bila shaka uelewa wako ni mdogo mno. Nachelea kusema kama ulienda shule basi ilikuwa ni kusindikiza wenzako tu na mwisho wa yote ulilamba kaSIFURI. Huenda hujui kusoma ndiyo maana unaandika upuuzi. Jifunze kusoma na kuandika kisha rejea kusoma kilichoandikwa na Babu Arfi, Kipenzi cha wana Mpanda.
ReplyDeleteAidha, kichwa chako na akili yako ilivyofinyu 'udini' umekutawala.
Ninampongeza kwa dhati Mhe Arfi kwa kuchukua uamuzi huo japo naona kama kidogo amechelewa maana hili lilionekana toka zamani sana sasa sijui huenda alikua akivumilia ama vipi. Na kama ni kuvumilia basi pia ninampongeza maana wenye mioyo ya uvumilivu kama yeye ni wachache.
Ushauri wangu kwako Mhe. ni kwamba fanya hima ujiondoe kabisa katika hicho chama cha kiimla maana hawachelewi kukufanyia kitu kibaya. Aidha, ninakushauri kwa saana kuwa Mchamungu wasijekukudhuru maana hao jamaa wamejizatiti katika sula la kutumia mabavu, watchout usijepigwa kitofali.
Nawasilisha.
NYINYI MNAO TANGULIZA DINI NA UKABILA KWENYE MIJADALA YA SIASA TANZANIA MNAITENGENEZEA NCHI HII UBOKO HARAM USIO HITAJIKA,MNA FANYA DINI AU KABILA YA MTU NDIO CHETI CHA KUONGOZA AU DIGIRII SASA MTAKUJA JUTA PALE MTAKAPO MCHAGUA MTU MWENYE JINA LA KIKRISTO NA KUSALI NAE KANISANI KUMBE NI MUISLAMU AU HANA DINI AMEFANYA HIVYO ILI APATE ULAJI.
ReplyDeleteACHENI UPUUZI WENYE KULITAFUTIA TAIFA MAJANGA KAMA UNAIPENDA DINI YAKO KWA NINI HUWI PADRI AU SHEHE UNATAKA SIASA ULAZIMISHE WATU WENGINE YASIO WAHUSU.
NA KAMA UNALIPENDA KABILA LAKO NENDA UKATAWAZWE UCHIFU HUKO ULIKOTOKA HILI NI TAIFA LA WENGI NA KIGEZO NI USHIRIKIANO SIO UTENGANO.
MDAU.
ALBANIA.
Sikushangaa kuona Arfi akiondoka kwani ni mnafiki na mchumia tumbo kama Zitto. Hapa hakuna cha uchaga wala uislam bali njaa na kigeugeu cha Arfi na Zitto na genge lao. Zitto anajiona kama ndiye mtanzania pekee anayeweza kuwa rais wakati ni mhuni wa kawaida na mbabaishaji kama waliopo CCM. SI warejee kwao CCM walikokuwa wakijiuza siku zote.
ReplyDeleteKwa kweli watanzania wenzangu mnatia aibu. Mnashindwa kuliona hili kuwa ni tatizo. Yaani chama kizima hakina watu wengine wanaoweza kuongoza chama ila mtu na mkwe wake. Kweli jamani hiki nichama cha mtei na wachagga au chama cha siasa. CCM inamapungufu yake, lakini watanzania mkichagua Chadema mtajuta kuzaliwa.
ReplyDeleteHistoria ni kitu kikubwa, jee unakumbuka wakati wa harakati za kugombea uhuru wetu, wakina MANGI fulani walikuwa wanapinga TANU. Na jamaa maarufu mmmoja wa waloanzisha chama aliwahi kusema kwa midh-haka kuwa wakizidi kutupa matatizo we will move the northern boundary and exclude them from our country.
ReplyDeleteWewe ni mamluki wa CCM. Toka kabisa Chadema rudi CCM. mtoto wa mkulima atakupokea kwa mikono miwili. Huko CCM utakuta kuwa muasisi wa chama hicho katika uhai wake ndiye alikuwa anachagua viongozi la sivyo Malecela angekuwa Rais. Mnafiki ni wewe na wana CCM wenzako.
ReplyDeleteKila mtu ana haki kufanya maamuzi ambayo anaona kwake ni sawa na yanamridhisha yeye na taasisi yake (wananchi waliomchagua). Pia maamuzi hayo yatakuwa na uzito na maana nzuri kama yatakuwa ni ya kweli na kufuata taratibu zote za kisheria katika taasisi husika.
ReplyDeleteSwala la bwana Arfi nalikubali na kulipongeza kwani amechukua maamuzi magumu kwa mtu aliye katika nafasi hiyo. Ila kwa mtazamo maneno yake mengine katika kufikisha huo ujumbe yanaweza kupunguza uzito wa ujumbe wake na kuonekana labda ana hasira au ana chuki binfsi au labda kuna maslahi anaona atapoteza kutokana na maamuzi ya hicho chama siku za karibuni.
1. Kulikuwa hakuna haja ya kusema anachaguliwa marafiki...hii inaonyesha ana weakness....umri wake binafsi ni upeo mkubwa wa kuchagulia watu marafiki badala ya wewe kuchaguliwa marafiki...pointless
2. Unafiki...fafanua ili ueleweke vizuri na hao wanafiki uwaanike hadharani
3. Katika ujumbe wake ametumia neno kama "kwenu" , "mmechukizwa" nani haswa anayemmaanisha au anayewaamanisha? angesema wazi...kama ni viongozi na ni viongozi gani...ingekisaidia chama ambacho bado yeye ni mwanachama.
Wasiwasi wangu mwingine je ni kweli anamaanisha hayo au labda hakupendezwa na maamuzi ya ya kikao ya kuwavua uongozi hao vijana watatu...maana swala lake anasema ni la muda mrefu...sasa iweje maamuzi haya ayatoe baada ya hao vijana kuviliwa uongozi? Nina shauku.
Mwisho kabisa napongeza maamuzi yake na kuyaheshimu...na kama ana nia nzuri na chama chake basi..pasi na shaka ataendelea kukijenga katika misingi sahihi. Tunahitaji viongozi imara na taasisi imara.
ReplyDeleteHaloo nafurahi sana jinsi wachagga wanavyo tikisa nchi ndo raha ya kusoma na kua na akili sasa nyie sijui na makabila yenu mnafanya nini?? mtuacha miaka 10000000 wala hatu hitaji chadema sema tumechoka na mambo ya CCM mtu alie enda shule lazima ana elewa maana ya kuchoka na CCM yaani hadi leo tuna gesi lakini bado umeme wa mgao sijui hyo gesi isinge kuwepo ingekuaje alafu bado mijinga inapiga kelele eti sijui chadema mara ccm think big Tanzania needs some changes
Huyu ndie M2 kwa vyovyote vile! Safi sana CDM ondoa MAGOGO yote kwamni ni mapandikizi ya CCM na walikuwa wamepangwa kuua CDM!Mungu kawaumbua peupeeeeeeeeee!
ReplyDeleteNdugu zangu watanzania tujadiliane hoja za kujenga na kuimarisha utanzania wetu ambao umejengwa kwenye misingi ya upendo,undugu na kuheshimiana tusiwe watu wa jazba na wenye mitazamo ya kutugawa kwa namna yoyote ile tuache mambo ya dini nje ya siasa Mungu awabariki nyote !!
ReplyDeleteLoh, kaaazi kweli kweli, sasa magenge ya wahuni yanataka kuchukua injiiii, hivyo msioafiki au wenye mawazo tofauti lazima tuwaweke OUT. Jina la chama ni cha DEMOKRASIA lakini kisicho na demokrasia. Ninadhani watanzania hawawezi kuacha kuongelea udini na ukabila wakati ni dumisho na mikakati ya siri ya chama, tumeona muda mrefu hata kwenye wabunge wa kuteuliwa hata mwanza tu penye wasukuma wengi wasomi lakini wanatoka kulekule, sasa ole wenu tuchukue inji NDIO MTATUKOMA KABISA, pole Zito kwa kuwa mwanachama wa chama kisicho na demokrasia na kuheshimu mawazo yako, ULIYATAKA MWENYEWE
ReplyDeleteDuuuu!
ReplyDeleteMambo ya kuvuta b....,halafu unakurupuka kuanza kufukuza viongozi bila hekima,mkiingia Ikulu si itakuwa balaa!
ReplyDelete