Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada ya leo (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza Msumbiji mabao 5-1.
Mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati mengine yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia Minja.
Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho Jumapili (Novemba 10 mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
Tanzanite inayofundishwa na Rogasian Kaijage itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini.
Mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 6 na 8 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22 mwaka huu.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Mtuuuumeeeee na kama watafanikiwa kucheza kombe la dunia hawa dada zetu,basi hiyo timu ya wanaume inayoitwa TAIFA STARS ifutwe maana tumechoka kuaibishwa miaka nenda miaka ludi,,naitwa mdudu kakakuona nipo huku UINGEREZA.
ReplyDeleteKwanza natoa hongera kwa wachezaji wa timu hii kwa ushindi mnono.
ReplyDeleteMajina ya hawa 'first eleven' ya Tanzanite U-20 women team walioanza mechi hii leo ktk picha ni nani na nani,blogu-ya-jamii mlete taarifa fupi lakini iliyosheheni 'data' ili kutofautisha na vyombo vingine ya tekenolojia ya habari na mawasiliano.