Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani wakiwasili katika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kupata maelezo ya Tovuti Kuu ya Serikali kabla ya kuizindua tovuti hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tovuti Kuu ya Serikali www.tanzania.go.tz itakayowawezesha wananchi kupata taarifa na huduma mbalimbali za serikali kwa urahisi, haraka na kwa wakati. Wanaoshuhudia kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani na Dkt. Jabiri Bakari ,Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao ambao ni wasimamizi wa Tovuti hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifurahia jambo mara baada ya kuzindua Tovuti Kuu ya Serikali na kuwataka wananchi kuitumia katika kupata taarifa mbalimbali za serikali.
BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI
BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...