Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya ZAYADESA Bi. Lucy Majaliwa akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya siku tano ya utoaji huduma za Afya kwa watu wa makundi maalum (KPS) Bi. Zainab Udi kutoka kitengo cha ushauri nasaha na upimaji wa VVU Mnazi Mmoja Hospitali.
Afisa mipango wa Jumuiya ya ZAYEDESA Aisha Ali Karume akimkaribisha mgeni rasmin Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya ZAYADESA Bi. Lucy Majaliwa katika ufungaji wa mafunzo ya utoaji huduma za Afya kwa watu wa makundi maalum (KPS) huko Ofisini kwao Miembeni Mjini Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya ZAYADESA Bi. Lucy Majaliwa akitoa nasaha mara baada ya kufunga mafunzo ya utoaji huduma za Afya kwa watu wa makundi maalum (KPS) yaliyofanyika Ofisini kwao Miembeni Mjini Zanzibar (kulia) Muezeshaji kutoka Wizara ya Afya Shaaban Hassan Haji.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya utoaji huduma za Afya kwa watu wa makundi maalum (KPS) wakimsikiliza kwa makini Katibu mtendaji wa Jumuiya ya ZAYADESA Bi. Lucy Majaliwa (hayupo pichan) wakati wa ufungaji wa mafunzo yao ya siku tano huko Ofisini kwao Miembeni Mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...