Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini , Afande Pius Nyambacha ( aliyesimama) akisoma maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa ,kufungua kikao  cha kazi cha Makamanda wa Mikoa na makao makuu wa  Jeshi hilo  leo katika ukumbi wa Hoteli ya Edema ya Mjini hapa ( wapili kutoka kulia) ni Naibu Kamishina Jenereli wa Jeshi hilo nchini, Lidwino Simon Mgumba.
 Baadhi ya Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimsililiza mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa  ( hayupo pichani), leo  wakati wa  kufungua kikao cha kazi cha Maofisa wa ngazi za juu  na Makamanda wa Mikoa  pamoja na watumishi raia katika ukumbi wa Hoteli ya Edema, ya Mjini Morogoro
 Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akifungua kikao cha kazi cha Maofisa wa ngazi za juu  na Makamanda wa Mikoa  pamoja na watumishi raia katika ukumbi wa Hoteli ya Edema, ya Mjini Morogoro
Juu na chini ni Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Lilian Mapfa ( kati kati walioketi) katika   picha ya pamoja na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji , Pius Nyambacha ( wanne kushoto) na ( watatu kutoka kulia ) ni  Naibu Kamishina wa Jeshi hilo, Lidwino  Simon Mgumba,  pamoja na wageni waalikwa kutoka Idara ya Uhamiaji,  Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro sambamba na Makamanda wa Mikoa wa Jeshi hilo , mara baada ya Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, baada ya kufungua kikao cha kazi  Novemba 11, mwaka huu ukumbi wa Hoteli ya Edema, ya Mjini Morogoro. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Laptop zinatumika hadi kwenye Majeshi ya Zimamoto?

    Kwa kasi hii ya Dijitali kwa akina Sajenti Marwa kuweza ku 'browse' nchini mnapo haribu mtatafutwa kwa mtandao ni muda wa ninyi Wahalifu mkalime!!!!

    Uhalifu sasa basi!

    ReplyDelete
  2. Mnapobisha mkisema Miaka zaidi ya 50 ya Uhuru Tanzania hakuna maendeleo nakataa,,, Polisi iliyokuwa inajulikana kwa matumizi makubwa ya makabrasha na makaratasi sasa inatumia Laptop na internet!!

    ReplyDelete
  3. Wengi hubisha kwa nongwa na bila vigezo!!!

    Sasa Polisi wanatumia Laptop?

    Mkisema Jakaya Kikwete hajaleta Maendeleo Tanzania mtakuwa wanafiki kama ''Coalition of the willing'' katika Afrika ya Mashariki!

    ReplyDelete
  4. Arooo Afande Kyaruzi !!!

    Rogi in kwenye inteneti haraka, ngoja niri tafute Riharifu katika FESIBUKU nikiri kosa humo nitarukia kwenye ISNTAGRAMU na kama rikini toroka NITA SIKANI picha yake na KUIEDITI na hapo ni razima tutari aresiti tu KIDIJITALI!!!

    ReplyDelete
  5. Ohhh!

    Netiweki bado ipo chini, uripo kuja kuripoti hapa Polisi Positi nirianza kuritafuta rifaili rako online.

    Rakini nitajitahidi kuripata Mutandaoni Fairi rako Rabda uniongezee Vocha !!!

    ReplyDelete
  6. Laptop ya mkufunzi au mtoa mada. Naona makanda wote wana kalamu na notepad na maji madogo ya kilimanjaro. Polisi bado hawajawezeshwa vya kutosha kupata vifaa vya kisasa kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu. Hata barabarani unakuta wako patrol hawana redio. Polisi wote wanatakiwa wapewe redio call....

    ReplyDelete
  7. Kuna chama kimoja cha siasa chenye kudai kuwa tangu uhuru Tanzania hakuna hata tone la maendeleo; yaani, hakuna maendeleo yeyote.

    Na mbumbumbu wanakisikiliza bila kujibu mapigo kwa kuwa kiongozi wake kasema hivyo.

    Je kuwa na vyama vingi vya siasa sio maendeleo (political development)?

    Shame on you, chama hicho!

    Usiminye, Michuzi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...