Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Design Plus Mustaffa Maulid, kushoto akiwa na wagazi wengine wa kampuni hiyo wakiangalia moja ya yajongo ambayo yamejengwa kinyume cha sheria na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa maeneo ya kariakoo majengo hayo yako kiwanja no 11 na 12.
Huu ni Utaalam uliotukuka wa Ujenzi wa Majengo marefu yaliopo eneo la Kariakoo,jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. HATARI SANA,jengo moja likishika moto linateketea na mwenzake

    ReplyDelete
  2. Mfano mmoja wapo wa madhara halisi ya Rushwa wahusika wachache wenye kutoa kibali wamepokea rushwa na siku moja ikitokea janga kama moto litagharimu sana maisha na mali za watu. MUNGU TUSAIDIE.

    ReplyDelete
  3. Ningependa kuuliza kwamba hakika wahusika wameliona na wanafahamu namna walivyovunja sheria na kuhatarisha maisha ya watu kwa majengo hatari kama haya kariakoo,JE YATABOMOLEWA?

    ReplyDelete
  4. Ukweli inatisha. Vilevile angalia majengo yanayotizamana na J Mall mtaa wa Samora.

    ReplyDelete
  5. Hili jengo la kulia lazima lianguke !!!chonde chonde wakazi jengo la kulia hameni

    ReplyDelete
  6. Waziri anae husika na hiyo wizara ajiuzulu mara moja,na kama kuna meya au mkuu wa mkoa wawajibike wenyewe kabla ya kuchukuliwa sheria kali na kufungwa,,jamani hivi ni nn maana ya kuwa kiongozi,,yaani niaibu kubwa hatuwa hazichukuliwi mpaka hayo magofu ya umati wa watu,,na uongozi wenyewe ndio kama huo bora msiende MAKANISANI na MISIKITINI maana njia ya motoni iko wazi kwenu,

    ReplyDelete
  7. hivi kweli, kwanini hii imeletwa wakati majengo yamemalizika.

    Hivi hakuna aliyeona kwanzia majengo yanapandishwa? Mpaka yamefikia kiwango cha kuanza kupiga lipu?

    tutafika kweli?

    ni hayo tu
    Msemakweli

    ReplyDelete
  8. Ni aibu sana kusema nchi hii ina town planners na kuna master plan. Hivi aliepitisha hiyo ramani alisaidiwa kuipitia yeye kazi yake ikawa ni kuweka signature tu???????
    Aibu sanasanan, Mama Yetu Tibaijuka, tunajua una mengi sana ya kurekebisha katika wizara yako lakini kabla hujarekebisha majengo rekebisha watendaji wako na hakikisha kila aliehusika na utoaji vibali kinyume na taratibu unamuondoa. Kisingizio cha kuwa hatuna wataalamu wa kutosha kiachwe. Hii ni sector nyeti sana kama nchi haina ajirini katika soko la afrika mashariki wapo. Mbona watanzania wengi wameajiriwa nje ya nchi hii iweje sie tung'ang'anie kuwa hatuna wataalamu??????

    ReplyDelete
  9. MBONA HUKU KUKURUPUKA HAKUISHI TUUU?? KWANINI WAHUSIKA WANAKAA KIMYA HADI MAJENGO YANAMALIZIKA KUJENGWA NDO PURUKUSHANI YA KUHISI YAMEJENGWA VIBAY IANZE?? NATAMANI SHERIA KALI INGEKUWEPO NA KUTEKELEZWA, KAMA UCHINA, HAYA MAPUNGUFU KATIKA MAJENGO YANGEKOMA. HATUWEZI KUENDELEA KULEA UOVE KAMA HUU...JK WAWAJIBISHE WOTE HADHARANI-IWE FUNDISHO KWA WATENDAJI WAZEMBE NCHINI.

    ReplyDelete
  10. Wakati mchakato wa kuvunja 'maana ni hati hati' inawezekana Wahusika wakatoa Rushwa halafu Zoezi zikasitishwa.

    Mambo ya muhimu ni:

    1.MTOE LIFE JACKETS (MIAVULI YA KUJIOKOA )KWA WAKAZI WOTE WA MAJENGO HAYO KWA TAHADHARI ILI WAWEZE KURUKA KAMA ABIRIA WA NDEGE PINDI DHARURA AMA AJALI IKITOKEA!

    2.MUWEKE MITUNG YA ZIMA MOTO (FIRE EXTINGUISHERS).

    3.SERIKALI MTOE BIMA YA MAISHA KWA WAKAZI WOTE WA MAJENGO HAYO NA MALI ZAO.
    (GOVERNMNT COMPLETE COVER LIFE AND PROPERTY INSURANCE)

    ReplyDelete
  11. Wajameni Masuala madogo saana ya ya Majengo yetu yanatutoa kamasi tunashindwa kuwawajibisha a kuwajibishana , sasa yatakuwa mambo neti kama Sakata hili la kutengwa ktk Afrika ya Mashariki dhidi ya majirani zetu?

    Itabidi tufunge Mikanda ukubwa ni jiwe !

    ReplyDelete
  12. Tanzania!

    Ama kweli rushwa ni msingi mkuu wa maisha Tanzania.

    ReplyDelete
  13. Tunapata madhahara sasa hivi kwa sababu ya corrupt gorvernment iliyokithiri ndo mana kila sehemu kuna moshi.Signs tunazozion kila mahali kwenye ufisadi mara visiwa vya jersey, uswisi, madawa ,ujambazi, siraha zilizozagaa,ujenzi holela, you name it ni matokeo ya corrupt system ndo maana mbio zoooote hazitafaa kama hatutapigana na janga la Rushwa.

    ReplyDelete
  14. MMMM MIMI NAPITA TU!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. Nani anauliza mbona yalijengwa! Kwa sababu rushwa ilitolewa! Sasa wanaona itawatokea puani wanaanzaa kujitokeza kidogo kidogo! Tuone kama watafanya kitu! Kama kweli wanajali niambieni hayo majengo yakivunjwa. Yataegeshwa hivyo hivyo miaka 50 ijayo matokeo yake tasikika tu kwenye vyombo vya habari ndani na nje!

    ReplyDelete
  16. mlikataa sera za nyerere, kazi kwenu. yanawarudia...

    ReplyDelete
  17. Bado tuko kwenye ujamaa na kijitegemea. hakuna developers kwa sababu ardhi ya serikali.

    ReplyDelete
  18. Hao nao waganga njaa tu, wakaguzi gani amabao wenyewe nao hata kanuni za usalama hawajui; ona kati yao hamna hata mmoja aliye na safety gear ili hali wanataka wenzao wasimamie usalama.Safisha kwako kwanza kabla ya kuangalia kwa jirani. Jiji tupo na tunafanya kazi zetu ipasavyo.

    ReplyDelete
  19. Kama jamaa hawa wamevunja sheria, kama ni wajanja tu ama wamelipa rushwa kuficha madhambi yao, sioni kama kuna matatizo makubwa. NYUNDO.

    ReplyDelete
  20. Mbona huku Ulaya nilipo magorofa yamebanana kama hyo pichani???teh teh teh....issue hapo ni yawe ya quality baaasi; pili kuwe na uwezo wa kuzima moto pindi unapotokea....kubanana sio inshu...mjini hapo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...