Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nafikiri mawazo ya baba wa taifa ni mazuri kwa wakati ule. Ili nchi iendelee sasa tunahitaji kuwekeza katika ardhi tuliokuwa nayo. Jukumu la serikali litakuwa kulinda raia ili wasiwe watwana. Hii imewezekana katika nchi zilizoendelea. Raia asiyejiweza anasaidiwa na serikali. Hivyo serikali jukumu lake la kukusanya kodi na kuwasaidia raia wasiokuwa na kazi au mali. Hivyo ushauri wangu ni kuwa serikali iazishe "WELFARE SYSTEM" na ardhi ipewe wawekezaji. Nafikiri wakati umefika kuanzisha "WELFARE SYSTEM" ili kulinda raia na nchi kupata maendeleo.

    ReplyDelete
  2. Hewala baba umenena. That is exactly what is happening. Pia utapeli mkubwa viwanja kuwa na hati mbili mbili. Watu kudhulumiwa,kukimbilia utajiri ,maskini kubaki maskini. Nchi imegawanyika vibaya sana. Wenye nacho na wasio nacho. Mie nilitapeliwa vibaya sana kiwanja changu na hiyo deal ilisukwa maana hata wizara ya ardhi karatasi zangu zilideletiwa zote zikawa added za mtapeli mwenzao. Nimefuatilia mpaka nimechoka nisije katwa shingo kisa kiwanja.Ila Mumbai anaona. Mtu yoyote anayemdhulumu mwenzie hata shilingi moja mungu anamuona. Asante baba wa taifa. Tutakukumbuka daima.

    ReplyDelete
  3. Hapa Mwalimu ilisema jambo kubwa mno, isipokuwa mimi naamini kuwa mtu hawezi kuuza ardhi, kwani ardhi ni mali ya uma, mali yetu sote.Ni mali yetu tulio hapa leo na ni mali ya hao watakaozaliwa na kuishi baada yetu.Hao wanaonunua ardhi sifikiri kama watakuwa na mabavu ya kuzuia wajukuu wa wajukuu wetu kudai ardhi yao, na watakuwa na ruhusa ya kuchukua matofali yao,na wakichafua ardhi wananchi watawanyoa nywele.

    ReplyDelete
  4. Ujumbe huu wa Hayati Kambarage Nyerere wanatakiwa akina Kagame Museveni na Kenyatta watumiwe ili waelewe ni kwa nini Tanzania inakataa ardhi kuwa ktk Afrika ya Mashariki!

    Kopi yake ya Ujumbe pia atumiwe Katibu Mkuu wa Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera.

    Nafikiri wakizipata ndio watatuelewa Watanzania na msimamo wetu.

    Je, kwa makosa yao hawaoni ni kwani nini wao Kenya, Uganda na Rwanda wana uhaba wa ardhi na sasa wanainyemelea ya Tanzania?

    ReplyDelete
  5. Maneno Makubwa sana!

    Hivi anayedai anaimiliki ardhi kama shati lake, hivi

    1.Pana mtu yeyote alizaliwa akiwa amekuja duniani na umiliki wa ardhi hata ukubwa wa Kaburi?

    2.Pana mtu yeyote ambaye amezaliwa na Bunda la Noti mkononi?

    3.Hivi kweli pana mtu yeyote anaweza kuzikwa Kaburini na Hati miliki ya ardhi anayoimiliki ama Bunda la Noti anazomiliki ?

    JIBU KWA HAYO MATATU (3) NI HAPANA HIVYO ARDHI NI MALI YA SERIKALI ILI MIMI NA WEWE TUKIFA SERIKALI INAIMILIKISHA ARDHI ILIYO ACHWA NA ALIYEKUFA KWA WALIO HAI WANAO ENDELEA NA MAISHA NA WENYE KUTAKA KUITUMIA !!!

    ReplyDelete
  6. Hayati J.K Nyerere !

    Wewe katika Uhai wako ulimtwanga Iddi Amini Raisi wa Uganda mwaka 1978-79 huku mwaka huu 2013 Mwanao J.K-Jakaya Kikwete AMEENDELEZA HESHIMA amewatwanga vibaya saaana Majeshi ya Msituni ya M-23 ya Maraisi Wawili Majambazi wa Vita Kagame Rwanda wa na Museveni wa Uganda!!!

    ReplyDelete
  7. ni kweli kabisa aliyosema baba wa taifa na ndo yanayoonekana hivi sasa na yanayoendelea wakuu wetu kuza ardhi kiholela holela kwa wageni na watanganyika tupo watwana katika nchi yetu na mwishowe tunakimbia nchi yetu na kwenda majuu na kuwa wabeba maboksi.
    i miss baba wetu wa taifa uliona mbali baba mungu akubariki huko ulipo uliyoyasema ni kweli kabisa na ndo yanayotokea hivi sasa

    ReplyDelete
  8. Huyu Mzee wa busara sana. Angalieni Kenya, Rwanda na Uganda wataiba ardhi yenu!

    ReplyDelete
  9. Ukisoma hotuba ya Kennedy ya 1960 wakati Marekani inaleta welfare system kwa watu waliokosa kazi kwa sababu ya mashine unaona ndiyo solution kwa nchi kama zetu zenye unemployment kubwa na uwezo mdogo wa kutengeneza ajira. Lakini swala ni Je tunaweza kuafford social welfare system hii wakati tuko milioni arobaini ndio issue, mapato yetu yanatosha kulipa matumizi ya kawaida ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara na madeni ya ndani na nje. Welfare hii ingeongeza purchasing power ya wananchi, na consumption ikiwa ni pamoja na public expenditure katika bidhaa na hivyo kuchangia kukuza uchumi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...