Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO inasema dunia itakuwa na upungufu wa wafanyakazi milioni 12.9 katika sekta ya afya ifikapo mwaka 2035, huku kwa sasa upungufu huo ni milioni 7.2, . Serikali yaTanzaniainakiri upungufu huo kuikabili sekta ya afya na kuelezea mikakati iliyopo katika kukabilina na upungufu wa wafanya kazi wa sekta ya afya kwa kuongeza vyuo vya udaktari na kuendesha sekta hiyo kibishara.Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa naibu waziri wa afya wa Tanzania Dk Seif Rashid (pichani) anasema mikakati hiyo inakabiliana na ongezeko la magonjwa na ajali lakini kwanza anaanza kuainisha mikakati ya kielimu.
Kusikiliza mahojiano hayo baina ya Radio ya Umoja wa Mataifa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid BOFYA HAPA:
http://www.unmultimedia.org/


Umejitahidi waziri,
ReplyDeleteLakini inasikitisha kama naibu waziri wa afya anaweza zungumzia njia mbadala za kuweza ongeza ufanisi kwenye huduma za afya bila kuongelea njia za kujikinga au kuzuia magonjwa mbalimbali, na nini wizara inafanya kupunguza magonjwa hasa hayo yasiyoambukizwa na ajali kwa ujumla wake.
Amenisikitisha sana aliposema vituo vya afya vinatakiwa kuendeshwa kibiashara, bila kugusia ni vipi watanzania wa kipato cha chini wataweza kupata huduma kwenye hivyo vituo.
Kwa bima ya afya, ni rahisi kusema watu wajiunge, lakini je mtu wa kule Magu ni vipi tutamsaidia alipie hiyo bima. Na hii bima ya afya ni katika mfumo wa sasa wa NHIF na CHF/TIKA au kutakuwa na mabadiliko, maana mfumo wa sasa una mapungufu makubwa.
Vile vile siyo sahihi kusema vituo vya afya viendeshwe kibiashara...nafikiri labda alikuwa anamaanisha kuongeza ufanisi. Haiwezekani tukaifanya afya kuwa commodity kama ambavyo tunanunua gari, au kununua vitu super market.
Waziri ana ideas nzuri lakini anahitaji a good technical advisor kum-guide, la sivyo tunaelekea pabaya!