Raia wa China wamekamatwa jijini Dar es Salaam maeneo ya Mikocheni wakiwa na shehena ya vipande 700 vya meno ya tembo. Wakazi wa eneo hilo wanaowafahamu Wachina hao wamesema huwa wanawaona wakiuza ndimu na vitunguu. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Kaghasheki amesema inakadiriwa kuwa ni zaidi ya tembo 200 waliouawa ili kupata meno hayo. Akasema amemweleza mmoja wa Wachina hao kuwa ingelikuwa amekamatwa nchini kwao China, hukumu ambayo ingempasa ni kifo. 
Waziri pia alisema anahisi huenda watu hawa wakawa wanafahamu ama kuhusika na moja ya makontena yaliyokamatwa nchini China yakiwa na meno ya tembo. Habari zaidi, tizama video ifuatayo ya taarifa ya ITV.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Ipelekeni China hii video waone huko maana wanawanyanyasa ndugu zetu huko na madawa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tafadhali wanaoua tembo na wauza unga wote ni waharifu na wanatakiwa kufikishwa mbele ya sheria bila kujali rangi zao. Hivyo jitihada za pande zote, china na Tanzania zinastahili kupongezwa na kuungwa mkono na wananchi pande zote na dunia kwa ujumla wake.
      Tunakushukuru mhe. Waziri kwa jitihada zako wananchi tuko nyuma yako, tunamwamini Mhe. Rais wetu wala hakukosea kukuchagua ktk nafasi, chapa kazi.

      Delete
  2. Waziri Kagasheki anajitahidi sana katika kulinda mali asili zetu ila inavyoonekana hii vita anayopigana ni kubwa na ni ya vigogo haswa...ukiwaangalia sana hao wachina lazima watakua ni vidagaa tu na mapapa yenyewe hapo hamna ..sasa ni juu ya serikali kukamata hayo mapapa na ikibidi sheria ibadilike iwe ni hukumu ya kifo kwa makosa kama haya..mungu ibariki Tanzania.
    mdau wa UK

    ReplyDelete
  3. Meno 700 maana yake tembo 350 waliuwawa.

    ReplyDelete
  4. Jamani hawa wachina hawana hata huruma, ingekuwa ni watanzania wamekamatwa china wangenyongwa...yaani sina hata cha kusema

    ReplyDelete
  5. Wachina hawa "wafanyiwe" mbinu mpaka waeleze mtandao mzima toka walipopata haya meno,malipo na nani kalipa, nani kalipwa,wahusika wooote...hadi majangiri na sehemu walipouliwa tembo hawa maskini.Ni ishara nzuri kwa waziri sasa akiacha kulala na kuwajibika KI-MWAKYEMBE.Siku zote ulikuwa wapi? Asante mdogo wangu.

    ReplyDelete
  6. Mimba ya tembo ni miezi 19!! Kwa mwendo huu kweli miaka miwili ijayo tutakuwa na tembo!!!

    ReplyDelete
  7. wahusika wakuu ni watu ktk serikali ndio mapapa wenye kuhusika na uwindaji wa tembo sitegemei mchina atakuwa ameenda kuwinda yeye ameuziwa na watu wetu wenyewe na hao ndio wa kukamatwa na kuadhibiwa , hawa wachina wamefanywa kama chambo tu

    ReplyDelete
  8. Hongera Sana Mhe. Waziri, chapa kazi achana na wanaotaka umaarufu wa nadharia ya kupanga maneno ya kuongea ili waonekane kwenye tv kwa matakwa ya kukuza umaarufu wao wa kisiasa. Wananchi tuko na wewe na tunauona uzalendo Wako na uaminifu na heshima kubwa unayompatia Mhe. Rais wetu kwa kujali na kuheshimu kiapo na dhamana ya cheo alichokupatia kwa manufaa ya Taifa letu. Shaka ondoa kwani wewe Ni mmoja wa askari wa mwamvuri wanaomsaidia Mhe. Rais wetu kwa uaminifu na uzalendo wa hali ya juu ktk eneo lako la kazi, na wananchi tunaliona hili.

    ReplyDelete
  9. niliwataadharisha kuhusu wachina mwanzo kabisa wanaingia tanzania niliwaonya saaana na nikaomba selikali ikae macho na hawa wageni.

    ReplyDelete
  10. What is the punishment for killing a giant Panda in China??
    I guess the same punishment should be dished out to these ruthless people who have no respect to our nation and the hospitality offered to them. It's high time we start to scrutinize who we invite into our country and what are they doing.Otherwise future generation will only here about the beauty of country through books.

    ReplyDelete
  11. Ongera kwa kazi nzuri mh waziri ila isiwe nguvu ya soda kwani tunazo kesi za Epa na Bot na nyingine nyingi wahusika wanapigwa kalennda badala ya mvua.
    Kuhusu hawa nikwamba Wachina ni ndugu zetu kabisa kwani mabadiliko tuliyo nayo yanatokana na wachina na hasa kwa kuimalisha mawasiliano (simu) na usafiri Bodaboda hapa hatuwezi kuwachuki bali watusaidie kufahamu nani kawauzia hao watanzania ndo wakuchapa kiboko cha nguvu.Wachina wapewe adhabu kwa mjibu wa sheria ila mahusiano ya Tanzania na CHINA Chonde chonde msiguse kijijini panaendeka vizuri bodaboda na kasimu TECHINO. HAWA NISAWA NA WALE VIJANA WA KAUNGA Walo kamatwa china.Hii ni kazi ya mahakama na polisi.
    Ila wachina wazuri wanakaribishwa tufanye biashara.

    ReplyDelete
  12. wangekamatwa kwao china wangenyongwa,ila kwa hapa bongo hata wakipatikana na hatia sidhani kama watakaa jela zaidi ya miaka 3

    ReplyDelete
  13. our elephants are killed by our own people who sell the tusks to foreigners and others. They should be punished in the first place , however i dont agree with death penalty for this crime , that will be too much unfortunately , even if the punishment of killing a panda is death thats inhumane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...