Mwishoni wa wiki, Uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa mataifa, ulitembelewa na wanafunzi wanajeshi wanane wanaoshiriki katika mafunzo ya miezi kumi, kupitia International Fellows Program yanayotolewa United States Army War war College and Carlisle Barrace.
Chuo hicho ambacho kipo nchini Marekani, kila mwaka huanda mafunzo hayo katika ngazi ya maafisa kutoka mataifa mbalimbali marafiki.
Kwa mwaka huu, mafunzo hayo yanawanafunzi 367 kati yao 300 ni wamarekani na waliobaki 67 wanatoka katika mataifa mbalimbali ikiwamo Tanzania.
Wanafunzi hao walifika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kama sehemu ya ziara ya mafunzo ambapo pamoja na masuala mengine, walitaka kufahamu vipaumbele vya Tanzania katika masuala muhimu yanayoikabili dunia hivi sasa ikiwani ni pamoja na matatizo yanayotokana na Mabadiliko ya Tabia nchi na matatizo ya maji kwa Afrika na namna gani Tanzania kama sehemu ya Afrika imejipanga kukabiliana nayo.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza na sehemu ya wanafunzi wanajeshi wanaohudhuria mafunzo ya miezi kumi katika Chuo cha Kijeshi cha Marekani kupitia International Fellows Program, wanafunzi hao akiwamo Luteni Kanal Francis Ronald Mbindi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walifika katik Uwakilishi wa Kudumu ikiwa ni sehemu ya zaira ya mafunzo ili kujifunza masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo ni vipaumbele vya Tanzania. Kushoto kwa Balozi Manongi, ni Naibu Muwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi.
Muwakilishi wa Kudumu Balozi Manongi akisisitiza kwamba mabadiliko ya Tabia nchi ( Climate Change) si suala la nadharia kwa sababu yapo matukio mengi yanayoendelea hivi sasa duniani kote ambayo ni dhahiri yanatokana na mabadiliko hayo. akatolea mfano wa Tanzania ambako kumekuwapo na migogoro na hata mapigano ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji wakigombea ardhi, maji na malisho. Akasema migogoro kama hiyo ambayo inaathari kubwa kwa jamii za wafugaji na wakulima lakini pia hata kwa serikali kuu. Na kwamba inaweza kuonekana kama ni tatizo la eneo fulani au nchi fulani lakini kama likiangaliwa katika mapana yake dhahiri nyuma yake ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi. Hata hivyo akasema serikali ya Tanzania inajitahidi sana katika kujaribu kutafuta suluhu kuhusiana na tatizo hilo ambalo anaamini linatokea pia katika nchi nyingine hususani Afrika
Luten Kanali, Francis Ronald Mbindi kutoka JWTZ akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya mazungumzo yao na Uongozi wa Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
4.IMG-4708. Luteni Kanal Francis Mbindi akimkabidhi kwa niaba ya wenzake, Balozi Tuvako Manongi, sehemu ya hotuba maarufu ya Rais Abraham Lincolin aliyoitoa Novemba, 19, 1863 katika maadhimisho ya miaka 150 ya GettysBury ( The turning Point :the 150th Anniversary of the Gettysbury address) hotuba hiyo ya Rais Lincolin inayohesabika kama hotuba muhimu sana kuwahi kutolewa na Rais Lincolin ilikuwa ikielezea kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe ( CIVIL War). vita hivyo vilivyotokea katika eneo hilo la GettysBury vinaelezewa kama vita vilivyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu, ambapo inasadikiwa zaidi ya wanajeshi 50,000 waliathirika ama kwa kupoteza maisha, kuchukuliwa mateka, kujeruhiwa au hawakujulikana waliko

Wageni wetu wakipeana na kusaini kitabu cha wageni, hawa wote ni wanajeshi katika ngazi ya maafisa , hawakuhitaji kukaa mezani ili kusaini kitabu
Balozi Tuvako Manongi akiendelea kubadilishana mawazo na wageni wake, nyuma anayeonekana kwa mbali ni Balozi Ramadhan Mwinyi. HABARI NA PICHA NA MDAU MAURA MWINGIRA WA UWAKILISHI WA KUDUMU WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...