Warsha(WORKSHOP) inahusu UIGIZAJI KWA AJILI YA FILAMU(ACTING FOR FILM).
Mwezeshaji (FACILITATOR) ni AKPOR OTEBELE kutoka HAKIKA ENTERTAINMENT (TZ),Mary Birdi, Nasir Mohamed, Vernon Cloete, Imanuel Mnzava, Aneth Peter katika sehemu ya uigizaji katika filamu.
Vision For Youth pia wametoa warsha katika upande wa HIV/AIDS( hasa katika namna ya kuishi na virusi vya ukimwi, kuwa na familia, mahusiano na afya njema) .
Warsha imeandaliwa na HAKIKA ENTERTAINMENT ikishirikiana na ARUSHA AFRICAN FILM FESTIVAL.
Warsha inafanyika katika kumbi za ALLIANCE FRANCE Tarehe 25-26 November 2013 na kuendelea katika viwanja vya VIAVIA Tarehe 27-28 November 2013.
Washiriki wa Warsha hii ni waigizaji, wadau na wapenzi wa filamu kutoka Tanzania hasa Arusha na nje ya nchi. Idadi ya zaidi ya washirikin 40 watanufaika na warsha hii.
Pia washiriki watapata fursa ya kutengeneza filamu fupi ya Dakika 5-10 inyoelezea namna ya kuishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika jamii kwa Nyanja tajwa hapo juu.
Filamu hii fupi itaoneshwa siku ya tarehe 01/12 katika hitimisho la rasmi wa tamasha la filamu za Afrika la Arusha, ViaVia Cultural Café kuanzia saa 2 usiku.
Wageni Rasmi katika ufunguzi ni Mr. Allan Kijazi (Mkurugenzi Mkuu-TANAPA) na Mr. WILBARD CHAMBULO(mwenyekiti-TATO), Dr. Vicensia Shule(Mhadhiri wa Chuo kikuu UDSM)
Pia katika kipindi hiki cha AAFF kutakua na Warsha ya Sanaa ya Uandishi (Arts for Journalist) katika Ukumbi wa Makumbusho (National Natural History Museum) Arusha kuanzia tarehe 28-30/11/2013. Warsha hii inaandaliwa na Zanzibar Film Festival (ZIFF)
Warsha inayohusu UIGIZAJI KWA
AJILI YA FILAMU(ACTING FOR FILM) ikiendelea. Mwezeshaji (FACILITATOR) ni AKPOR OTEBELE kutoka HAKIKA
ENTERTAINMENT (TZ),Mary Birdi, Nasir Mohamed, Vernon Cloete, Imanuel Mnzava, Aneth
Peter katika sehemu ya uigizaji katika filamu.
Kazi nzuri sana kwa Hakika Entertainment..... Tunashukuru pia kwa kutupa nafasi Vision for Youth.
ReplyDeleteViolet
Vision for Youth