WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kila Halmashauri hapa nchini inapaswa kuweka kwenye mpango wake wa maendeleo kifungu cha ujenzi wa maktaba ya wilaya ili watu waweze kusoma na kujiendeleza kwa urahisi.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Novemba 16, 2013) wakati akiwahutubia washiriki wa mahafali ya 19 ya Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi wa Nyaraka cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.
Jumla ya wahitimu 749 walitunukiwa vyeti kati yao 244 vikiwa ni vya stashahada na 505 ni vya astahada katika fani za ukutubi na utunzaji nyaraka.
Alisema ukutubi ni mojawapo ya fani kongwe hapa duniani japo haiongelewi sana hapa nchini. “Hili ni eneo linalomgusa kila mmoja wetu, kuanzia mtu wa kawaida awe mkulima, mvuvi, seremala, mjasiriamali ama yeyote ambaye anahitaji taarifa mbalimbali zimsaidie katika maendeleo yake.
inasikitisha sana kuona jinsi gani viongozi wetu wana fikra ndogo.
ReplyDelete