Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizindua rasmi mradi wa umeme wa Berega.Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amezindua mradi mkubwa wa umeme uliopo katika kata Barega iliyopo katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Aidha alitembelea miradi mingine inayotekelezwa na MCC na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi. Pia alitembelea nyumba ambayo amewahi kuishi mwaka 1979 wakati akifanya utafiti wa miamba huko Kibaoni katika wilaya ya Mvomero ikiwa ni pamoja na kuonana na mwenyeji wake ambaye wameishi katika nyumba moja mwaka 1979-
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa Berega. Mradi huu umefadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo akisoma  taarifa ya hali ya umeme katika wilaya ya Kilosa kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
 Wakazi wa kata ya Berega iliyopo katika wilaya ya Kilosa wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ( hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...