Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel imewaasa Watanzania wote kote nchini kulinda amani na utulivu wa nchi katika kipindi hiki cha sikukuu ikiwa ni baada ya kuwatakia heri ya Christmas na mwaka mpya.

Akizungumza kwenye ofisi za makao makuu ya Airtel, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema sikukuu za Christmas na mwaka mpya ni sikukuu muhimu sana kwa wananchi wa taifa hili hivyo zinapaswa kusherehekewa kwa amani na utulivu.

“Ninawaomba wateja wa Airtel na watanzania wote kwa ujumla kutambua umuhimu wa sikukuu hizi na kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuhatarisha amani na utulivu wa taifa,” alisema Mmbando.

Aidha alisema katika msimu huu wa sikukuu bado Airtel inazidi kudhihirisha kuwa ni baba lao  kwa wateja wake kwa kutoa  huduma zilizo za gharama nafuu zinazowawezesha kutuma na kupokea pesa bure pia kutumia huduma mbalimbali za inataneti na kupiga kwenda mitandao yote.

“Airtel  bado ni baba lao kupitia huduma zetu mbalimbali, Wateja wetu bado wanaweza kunufaika na huduma zetu ambapo kwa sasa wateja wanaweza kupata vifurushi vya inataneti kwa gharama nafuu, kupiga simu kwenda mitandao yote na pia kutuma na kupokea pesa bure,” alisema Mmbando.

Ikumbukwe kuwa vifurishi vyote vya siku vya Yatosha vinadumu kwa masaa 25 tangu mteja anapojiunga ikiwa na lengo maalumu la kumfanya mteja aweze kufurahia huduma hiyo na kuwafaidisha watanzania waendelee kuokoa pesa nyingti walizokuwa wakizitumia kwenye mawasiliano na kuanza kuzitumia katika shughuli nyingine za uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...