Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa  Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
  Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva katika mazungumzo. Kushoto ni mkewe, Mama Mero
Picha ya pamoja Balozi Mero, Mama Mero na Bw. Azevedo.
-----
Mheshimiwa Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, amewasilisha hati za utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
 Katika mazungumzo,  Mkurugenzi Mkuu amemfahamisha Mh. Balozi  kuwa Shirika la Biashara Duniani liko katika hatua za mwisho ukamilisha majadiliano ya mikataba ya  Biashara ya Kimataifa katika maeneo matatu kwa pamoja  ikiwa ni masuala ya  Kilimo,  Maendeleo na  Uwezeshaji Biashara.
  Aidha,  Mkurungenzi Mkuu alielezea  mahusiano mazuri aliyonayo na nchi yetu kwa kipindi  kifupi akiwa kama Mkurugenzi Mkuu,  na  kuwa aliliona hilo wakati wa kampeini yake alipokuja nchini kuomba kura yetu. Ni kwa mantiki hiyo na imani aliyonayo kwa Tanzania, Mkurugenzi huyo ameomba Tanzania itumie ushawishi wake ili kufanikisha mkutano wa Mawaziri wa Biashara utakaofanyika mjini Bali, Indonesia, kuanzia tarehe 3-6 December 2013, ili kupitisha mikataba ya Biashara katika maeneo  matatu yaliyotajwa hapa juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...