Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania
Moezz Mir(wapili toka kulia)akimkabidhi msaada wa Mashine ya kupasha moto vifaa
vya hospitali kabla ya matumizi na baada ya matumizi kwa mgonjwa(Sterilizer) Mkurugenzi wa Zahanati
ya Njia Heath Centre ya Kiwalani jijini Dar es Salaam,Bw.Stephen Mosha(wapili
toka kushoto .Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali vyote vyenye thamani
ya shilingi Milioni 5,wengine
wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Utawala wa kituo hicho Bi,Hellen Olengailuva
na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya hiyo Christina Manyenye.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB
Tanzania Christina Manyenye ,akimkabidhi
Mwishehe Saidi ambaye ni mlemavu msaada wa mabati na saruji vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni
2.hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mwishehe Tabata jijijini Dar es Salaam.Msaada huo utamsaidia
kwa ajili ya ukarabati wa nyumba yake.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB
Tanzania Christina Manyenye akimkabidhi
Mwishehe Saidi ambaye ni mlemavu msaada wa mifuko ya Saruji 28,Mabati 18 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni
2.hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mwishehe Tabata jijijini Dar es Salaam.Msaada huo utamsaidia
kwa ajiri ya ukarabati wa nyumba yake.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania,akisoma hutuba kwa
wakazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam, wakati
wafanyakazi wa benki hiyo
walipofika kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni
5 katika Zahanati ya NJia Health Centre.Anayeshuhudia
(kushoto)ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Moezz Mir.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz
Mir akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Njia Health Centre,Bw. Stephen Mosha wakati
walipofika katika kituo hicho kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam,kutoa
msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya shilingi Milioni
5.Katikati ni Mkuu wa Utawala wa kituo hicho Bi,Hellen Olengailuva.
Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Njia Heath
Centre kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam,Bw Stephen Mosha ,akiongea na
waandishi wa habari wakati Uongozi wa
Benki ya KCB Tanzania,walipofika Hospitalini hapo kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali
vyenye thamani ya shilingi Milioni 5.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa benki hiyo Bw.Moezz Mir na
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Christina Manyenye.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...