Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba akiongea machache kuwashukuru Mbalozi wa wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumatano, Dec 11, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC nchini Marekani siku Bodi ya Utalii ilipotoa tuzo kwa mabalozi hao wanaotangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akiwashukuru mabalozi wa Utalii kabla ya kukabidhiwa tuzo zao kwa kazi nzuri wanaoifanya kwani sasa hizi Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka watalii wengi nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi akiongea machache kuelezea vivutio vingine vyilivyopo hifadhi za Taifa za wanyama pori na kuwashukuru Mabalozi hao kwa kazi nzuri ya kutangaza Utalii wa Tanzania.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...