Na Andrew Chale. 

DESEMBA 24 ‘kesho’ Jumanne kutakuwa hakutoshi ndani ya mgahawa na ukumbi wa kisasa wa Nyumbani Lounge kwenye bonge la ‘Party’ ya kuzaliwa kwa Mama Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous wa Khamsin, atakapokuwa akitimiza miaka 54. 
Party hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali wakiwemo wa filamu, muziki, mitindo na wabunifu. 
  Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashion, na muandaaji wa onyesho kubwa la Kila mwaka la Mavazi lijulikanalo kama … Usiku wa Khanga za Kale, anasema kuwa tayari mandalizi yameshakamilika na wadau mbali mbali wanatarajia kuhudhuria kwenye ‘party’ hiyo itakayokuwa ya aina yake. 
“Kesho Desemba 24, Ni siku yangu ya kuzaliwa, Namshukuru Mungu kwa neema zake kufika hadi leo hii kwa ulinzi na muongozo wake, leo hii mimi kufikia hapa na kutimiza miaka hii 54” alisema Asia Idarous. 
Akitoa nasaha zake kwa wabunifu wa mitindo wanaochipukia hapa nchini, Asia aliwataka wasivunjike moyo kwani kazi hiyo inahitaji uvumilivu na maalifa. “Namshukuru Mungu kwa kufikia hapa leo hii na hakika nitaendeleza fani hii pia nawaomba wabunifu na wanamitindo wanaochipukia kuwa na hali ya ushirikiano, kusaidiana, kuchapa kazi na kuwa na ‘tojo’ safi” alisema Asia Idarous Khamsin. 
Aidha, Asia Idarous alisema kuwa milango ipo wazi kwa wabunifu wa mitindo kupata ushahuri wake kwa watakaotaka huku akiwaombea wafike mbali katika kuendeleza gurudumu la mitindo hapa nchini.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. HONGERA SANA DADA YETU MWEMA ASIA IDAROUS KHAMSINI!

    Ni mfano mzuri sana unautoa kwetu kwa Kuadhimisha Siku ya Kuzaliwa kwa kuitaja Miaka Kamili ya kutimiza Miaka 54 kitu ambacho wengi wasio Majasiri kama wewe hawawezi!

    Maashallah, Mwenyezi akuzidishie zaidi!!!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana mama, kumbe umekula chumviee? Shikam Bibi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...