Mdau Franklin Mziray
Na Franklin Mziray 
Nimesoma maoni ya Maggid juu ya hotuba ya Rais wakati wa maziko ya Mzee Mandela. 
In deed Rais wetu amefunika kwa jinsi alivyotiririka na mchango wa taifa letu katika harakati za ukombozi si wa Afrika ya Kusini tu, bali bara zima. 
Nilitamani tu angeongeza kwamba tulifanya hivyo kwa uchache wa uwezo wetu kiuchumi na tulitumia kidogo tulichonacho kuwasaidia ndugu zetu.
Tulijijtolea kafara maendeleo ya uchumi wetu, tukapiga foleni kununua sabuni, acha sukari, ili tu wenzetu waweze kuwa huru, kuishi kama Waafrika na wenye haki ya nchi zao.
Sisi tunaokaa nje ya nchi aghalabu tunakutana na mijadala ya hali ya uchumi wa Tanzania kuwa dhaifu ama duni, lakini wanaotucheka wanasahau kwamba kicheko chao, kimetokana na sadaka zetu. JK Rais wangu umenifanya nijisikie Mtanzania mara zisizohesabika. Kama ulivyosema mwenye macho haambiwi ona au mwenye masikio asikie. Wale ambao hawakusikia au kuyaona hayo zamani, basi wamesikia. 
Kalale Pema Baba, babu na dira ya Afrika, Nelson Mandela. 
Nakumbuka 2001 uliponipa zawadi ya kitabu chako 'The Long Walk to Freedom' na kukinafsisha kwangu na maneno Best Wishes Franklin...



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...