Na Geofrey Tengeneza
Kundi la watalii 150 kutoka Israel limemaliza ziara yake ya siku hapa nchini na kuondoka kurejea nyumbani kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro baada ya ziara yao waliyoilezea kuwa ni ya mafaniko makubwa.
Waisrael hao walifika nchini kwa ndege maalumu ya watalii ya shirika la ndege la Israel (ELAL) ambayo ilizianza rasmi safari zake za moja kwa moja kutoka Tel Avivi Israel kuja KIA Tanzania tarehe 29/11/2013. Miongoni mwa watalii hao walikuwemo watu kumi (10) wenye ulemavu wa aina mbalimbali, na wandishi wa habari saba (7) kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Israel yakiwemo magazeti maarufu, kituo cha televisheni cha channel 10 ambacho ndiyo kikubwa nchini Israel na kituo cha televisheni cha channel 2.
Watalii ishirini na wanne (24) kati ya hao 150 wakiwemo walemavu wote kumi, walikuja mahsusi kwa jili ya kupanda mlima Kilimanjaro huku wapiga picha wa televisheni ya channel 10 wakipiga picha tukio hilo la aina yake. Walemavu hao kumi walifanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro hadi katika kituo cha Gilman. Watalii wengine waliosalia 126 walitembelea Hifadhi ya Taifa ya Manyara, Hifadhi ya Taifa Serengeti, Kreta ya Ngorongoro na baadae visiwa vya Zanzibar.
Akizungumza na wandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA, Mkurugenzi wa Kampuni ya utalii ya Safari Company ya nchini Israel iliyoratibu safari hiyo Bibi Ronit Hershkovitz amesema ziara hiyo pamoja na hatua ya shirika la ndege la Israel kuanzisha safari za moja kwa moja kuja KIA kutafungua milango ya Tanzania kuanza kupokea idadi kubwa ya watalii kutoka Israel.
Amesema ziara hiyo imekuwa ya kihistoria kwani wamefurahishwa sana na upekee wa vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini “ndugu zangu wa Israel wamefurahia sana na kushangazwa na uzuri wa vivutio vya kitalii vya Tanzania. Kwa mfano makundi ya simba kule Serengeti, wanyama maarufu watano (the big five) na mlima Kilimanjaro vimewasisimua sana” alisema bibi Hershkovitz.
Naye Meneja Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) mkoani Arusha Bw. Willy Lyimo aliwashukuru watalii hao toka Israel kwa kuja kutembelea vivutio vya Tanzania na akawataka wakawe mabalozi wema wa Tanzania nchini kwao. “ Mmejionea kwa macho yenu na kukiri uzuri wa vivutio vyetu, tunaomba mkawaambie ndugu zetu waisrael kuwa tunawakaribisha sana, na tunapenda kuwahikishia kuwa Tanzania ni nchi salama kabisa na yenye amani tele” alisema Bw. Lyimo.
Safari maalumu za watalii (charter flights) za shirika la ndege la Israel zitafanyika kila juma ya mwezi April, Mei, Julai, Agosti, Septemba na Desemba, hii ikimaanisha kuwa kutakuwa na safari nne kila mwezi uliotajwa hapo.
Baadahi ya watalii kutoka Israel wakifanyiwa ukaguzi katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) kabla ya kupanda ndege kurejea kwao Isreal.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Safari company ya nchini, Israel Ronit Hershkovitz akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kuzindua safari ya kwanza ya watalii 150 kutoka Israel kuja moja kwa moja Tanzania kupitia shirika la Ndege la ELAL la nchini humo.




Watalii mnakaribishwa nchini yetu haina matata.
ReplyDelete
ReplyDeleteHii ni habari nzuri na ya umuhimu mkubwa sana kwa historia ya taifa letu la Tanzania....mimi binafsi nafurahia sana kujua kuwa wa-Islael wamependa vivutio vyetu, uzuri wa nchi yetu, amani na utulivu wa Taifa letu;
Lakini kubwa zaidi ni kuwa ikiwa wao (wa-Iaslael) wanapenda vivutio vyetu na nchi yetu na hata kukubali kuanzisha safari za kitalii kama inavyosomeka hapo; ni ukweli usioweza kupingwa kuwa vivyo hivyo na sisi wa-Tanzania tunaweza kupata milango iliyofunguka huko Islael na kwenda kujionea vivutio vya ki-historia vilivyoko huko kwao, yaani kama ni kiutalii tu au hata kiimani pia.
Huu ndugu zangu ni ukurasa mpya sana.... na nataka kusisitiza kuwa aina yoyote ya uhusiano wa kirafiki baina ya Tanzania na Islael ni ishara mojawapo kuwa nchi yetu inakwenda kubarikiwa na MUNGU kwa kuwa hili ndungu zangu ni taifa teule la MUNGU - na maandiko hayatanguki - na hivyo kuwa na urafiki au na mahusiano mazuri na taifa kama hilo kuna siri kubwa ya mafanikio hapa.
Ukisoma katika maandiko matakatifu, na labda leo tuanze na Biblia, hasa Kitabu cha Mwanzo 12:3 – nanukuu "Nitawabariki wanaokubariki na yeyote anayekulaani nitamlaani; na watu wote duniani watabarikiwa kupitia wewe" hii nimetohoa toka New International Version (japo siyo tafsiri rasmi) lakini hata hivyo huko nako kwenye chanzo inasomeka hivii: Genesis 12:3 – I quote "I will bless those who bless you, and whoever curses you I will curse; and all peoples on earth will be blessed through you." (NIV)
Ukitaka kuchimba zaidi utaweza kugundua vitu vingi lakini ndugu zangu, ukijiuliza kwanini wakati wote mataifa makubwa duniani - labda niseme Marekani, hawajawahi kuwa kinyume na Islael (utaelewa tu) ....iko siri hapo, wanajua ziko baraka za MUNGU kupitia taifa hilo…..oooh!
Natamani……laiti kama siku moja Serikali ya Tanzania (baada ya kuweka sawa mambo yote ya ki-diplomasia) ingefungua ofisi za Ubalozi wa Islael hapa nchini....naamini huu utakuwa mwanzo wa Tanzania mpya. Na hapo nataka niseme kuwa watu wote wanaofuatilia nyakati za kibiblia pamoja na mambo yote ya kinabii watakubaliana nami kabisa kuwa Tanzania inahitaji sana mahusiano ya kibalozi na Islael…..MUNGU Ibariki Tanzania na Watu wake, Miaka 50 ijayo ya uhuru wetu iwe ya Baraka na Mfanikio – Amina!!!
Niombe radhi kwa upande wa “Admin” leo nimekuja kiimani zaidi…..lakini ni kwa nia njema tu …. mimi siwezi kuficha ndugu zangu, naipenda Tanzania…..na sababu ninayo, sina nchi nyingine zaidi ya Tanzania…huku nje tupo kwa muda tu lakini mwisho wa yote lazima kurudi nyumbani. Ingawa hivyo huu ni muono wangu na kuwa sifurahii kabisa wa-Tanzania wanaoiponda Tanzania kila siku ... ila mimi kwangu nchi yangu Tanzania (nyumbani) ni muhimu sana kuliko utajiri wanchi isiyo yangu. ....Lazime tupende kwetu wajemeni - Ankal unapo-post maendeleo ya mradi wa barabara za magari yaendayo kasi Dar pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali unanipa raha sana...siku moja uli-post ule "mkeka" toka Namtumbo kwenda.....nilipenda sana ile achilia mbali maendeleo ya daraja la Kigamboni na kule Malagalasi; lazima tupende kwetu bwana, kwanini?
Haukana cha Myahudi; hakuna cha mpagani; hakuna cha Mkurya, hakuna cha mchagga, hakuna cha chasaka, hakuna cha mhaya, hakuna cha mnyamaanga, hakuna cha Mtusi, hakuna cha Mhutu, Hakuna cha Mnyamukenge, hakuna cha aliyetahiriwa; hakuna cha asiyetahiriwa...wote tu watoto wa Mungu. Tukimwamini Mungu tunaitwa watoto warithi!
ReplyDelete