Mkuu wa kundi la Jahazi Modern Taarabu Mzee Yusuph,akikonga nyoyo za mashabi wake Tamasha la Taarabu lililofanyika katika Ukumbi wa Dar Live na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,mwishoni mwa wiki.
Wapiga kinandana na gitaa mashuhuru wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,kutoka kusho Father Mauji na Miraji Sultan,wakiburudisha mashabiki wao vilivyo katika Tamasha la Taarabu lililofanyika katika Ukumbi wa Dar Live,Chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania,mwishoni mwa wiki.
Mwanamziki wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,Khadija Yusuph akiwaburudisha mashabiki wake katika Tamasha la Taarabu lililofanyika katika Ukumbi wa Dar Live na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,mwishoni mwa wiki.
.jpg)
Shabiki wa muziki wa Taarabu Mohamed Haji akicheze vilivyo wakati Bi. Khadija Yusuph mwimbaji wa kundi la Jahazi Modern Taarabu akitumbuiza katika Tamasha la Taarabu lililofanyika kwenye Ukumbi wa Dar Live,chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania,mwishoni mwa wiki.
Mavazi gani haya jamani tena bi khadija huyo ahh basi tu kina mama hawajui jinsi gani mavazi ya vifuwa wazi yanakera kiasi gani.
ReplyDeleteDuh ! Angelijua asinge vaa hivyo.
ReplyDeletemavazi yanachefua roho haya dada jiheshimu uheshimiwe,
ReplyDeleteunajidharaulisha sanaaaaaaaaaa.
siku ya mwisho utajibu nini????
tafakari sana mauti ni wakati wowote hayangoji mtu tubia bado mapema.
Mavazi yaendane na mwili wandugu!
ReplyDeleteDa Khadija umzuri "Masha Allah" kadhalika sauti umejaaliwa si haba, lakini kumradhi kwa hili moja tu la kivazi, bora hata ungevaa lile 'buibui' letu la asili la 'ukaya' stara ingekuwepo kuliko hilo vazi ulilovaa hapo, au hata ungevaa hilo hilo, basi ukalitupia mtandio japo hapo kifuani tu, ukastiri hayo maungo. Hata hivyo ni ridhaa na pendekezo lako kipi uvae, lakini uzingatie ni kipi cha kukivaa khasa kwenye 'jahara' ya watu mithili hiyo. Narejea tena, samahani kama utakereka na maelezo yangu, kukumbushana ni wajibu na kutekeleza kila mtu na khiyari yake.
ReplyDelete