TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imeondolewa kwenye michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya baada ya kufungwa na timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali kwenye Uwanja wa Nyayo uliopo jijini Nairobi. Picha na GBL
Katika
mchezo huo, uliochezeshwa na refa Thiery Nkurunziza wa Burundi, aliyesaidiwa na
Idam Hamid wa Sudan na Mussie Kinde wa Ethiopia, hadi mapumziko, tayari wenyeji
walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa Thika
United, Clifton Miheso dakika ya nne kwa shuti la umbali wa mita 20, baada ya
kupokea pasi fupi ya Alan Wanga na kumchungulia kipa Ivo Mapunda.
Baada ya bao hilo, Stars walizinduka na kuanza kushambulia, lakini ukuta wa Kenya ulikuwa imara kuzuia mashambulizi yote.
Baada ya bao hilo, Stars walizinduka na kuanza kushambulia, lakini ukuta wa Kenya ulikuwa imara kuzuia mashambulizi yote.
Nafasi pekee nzuri ambayo Stars waliipata
ilikuwa dakika ya 44, wakati kona nzuri ya Mrisho Ngassa ilipopanguliwa na kipa
Duncan Ochieng, lakini Mbwana Samatta akachelewa kuunganisha, Joackins Atudo
akaondosha kwenye hatari.
Kipindi cha Stars ilicheza vizuri zaidi, lakini bado ukuta wa Harambee ulikuwa mgumu na nafasi pekee nzuri katika kipindi hicho ilikuwa dakika ya 88, wakati Mbwana Samatta alipomtoka beki wa Kenya na kuingia vizuri ndani ya 18, lakini akapiga juu.
Baada ya mchezo huo, wachezaji wa Stars walikuwa wakilia na ikabidi viongozi wachukue jukumu la kuwabembeleza. Nahidha Kevin Yondan ndiye alikuwa ana hali mbaya zaidi.
Kikosi cha Stars leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Michael Pius, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Hassan Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk65, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba/Farid Mussa dk65.
Kenya; Duncan Ochieng, Allan Wanga/Noa Wafula dk81, James Situma, Aboud Omar, Joackins Atudo, Peter Opiyo, Francis Kahata, Anthony Akumu, Clifton Miheso/Paul kiongera dk88, David Ochieng Owino na Edwin Lavatsa.

-MAHMOUD ZUBEIRY, NAIROBI

Kimsingi Stars hamkuweza "kutupa raha" watanzania, lakini siyo mbaya sana (japo ni mbaya, maana hamkutupa raha) .... kwahiyo, msilie sana vijana....ndo mchezo huo, unajua michezo ni afya, kudumisha mahusiano na ujirani mwema na siyo vita...nadhani bado mnayo nafasi-japokuwa sasa ndo mshatolewa hivyo....basi tusubiri tena mpaka 2014 ... ila hapo ndo majaaliwa ya MUNGU tena....tuwe na subira tu...ila kwakweli hamkutupa raha kabisaa....Yeah, kwahiyo angalau mkilia mnaonyesha kuwa mlitaka kufika mbali na pengine kuchukua ubingwa ila ridhki ndo haikuwa yetu...Jipime moyo tu, mpira utaendelea kudunda, si ndiyo vijana?
ReplyDeleteIla haitakuwa mbaya sana kama baadaye baadaye huko mbele (kama 2014 hivi) tuombe mechi ya kirafiki na Harambee Stars angalau tufute machozi na kuwaambia kuwa ile waliyotufunga (yani matokeo ya leo) aah walibahatisha tu...nadhani itakuwa imeweka mambo vizuri zaidi...tusingoje mpaka Challange Cup ijayo itakuwa too late hao tuwaombe "friend match" - (hapo naonyesha msisitizo) kisha tufute machozi kwa kuwa-dunga na siye vilevile....hawa wanafungika tu!
Kocha kiraka huyo
ReplyDeleteTimu ilicheza vizuri,ila ni wakati muafaka kwa wachezaji "Fulani Fulani" kuondolewa kwenye timu hii na ya Taifa kwa ujumla.
ReplyDeleteUshauri kwa Farid Musa-Wewe ni chipukizi mzuri sana,unapopewa nafasi na kocha onyesha kipaji chako,acha woga wa mechi ngumu na zenye tension kubwa kama ya jana,ndiyo unapata uzoefu hivyo.
David V
LEO ASUBUHI NIMEMSIKILIZA MTANGAZAJI MWANASIASA WA REDIO UHURU KIPINDI CHA MAPITIO YA MAGAZETI AKIWEKA SIASA KWA KUILAUMU KENYA KUWEKA MAJI YA MVUA KWENYE UWANJA! WATANZANIA TUNAPOZIDIWA TUJIFUNZE KUHESHIMU MATOKEO NA SIASA ZETU ZA KIPUUZI HAZITUSAIDII
ReplyDeletewakati umefika wa kuthamini makocha wazalendo tumeona mifano katika mashindano haya timu za wenzetu.Wapo wataalamu/makocha wazalendo-fanyeni utafiti.
ReplyDeletetusisahau pia kuwa hii pia ni biashara kenya ingetolewa basi na wakenya wasingekwenda uwanjani. hivyo ilikuwa sahihi tu .
ReplyDelete