Pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo mbele ya wananfunzi hao (hawapo pichani) baada ya kueleza kero zao. wengine kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa NJombe na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh.Deo Sanga kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge Mteule, Dk. Asha-Rose Migiro.
Ndugu Kinana na Ujumbe wake leo amekutana na Wanafunzi mbalimbali wa vyuo vya elimu ya juu mkoani humo na kusikiliza changamoto na kero zao mbalimbali na namna ya kuzifanyia kazi ikiwemo na kuzitatua.Kinana amefanya ziara maalum ya kikazi katika mkoa huo wa Njombe,baada ya kumaliza ziara yake ndefu ya mkoa wa Ruvuma na Mbeya,akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati kuu ya CCM,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Kama vile haitoshi leo jioni kabla ya kurejea jijini Dar kwa njia ya Treni ya TAZAR kutokea Makambako, Ndugu Kinana alishiriki uzinduzi wa albamu ya kikundi cha Sanaa za Vichekesho cha mjini Njombe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wanafunzi hao jioni ya leo katika chuo cha Maendeleo ya Jamii,kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakumba,mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mh,Sarah Dumba akitoa sehemu ya ufafanuzi kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo katika chuo cha Uuguzi Kibena,Mkoani Njombe wakati wa kujibu maswali ya wanafunzi wa chuo hicho kama waonekanavyo pichani.
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Iringa akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabiri mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake aliokuwa ameambatana nao.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...