Katibu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakipokelewa jijini Dar na Wanachama wa CCM,wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Dar-Es-Salaam,Ramadhan Madabida.
Ndugu Kinana akisalimiana na Wanachama wa CCM,mara baada ya kushuka kwenye treni ya TAZARA mapema leo asubuhi akitokea na Makambako.
Ndugu
Kinan akiagana na baadhi wanachama wa CCM,waliofika kumsabahi katika
kituo cha Mlimba,wakati treni hiyo ilipokuwa imesimama kwa ajili ya
kupakia na kushusha abiria ,Kinana aliongozana na Wajumbe wake,katibu wa
NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asha-Rose Migiro pamoja na
Katibu wa NEC,Itikadi n Uenezi,Nape Nnauye wakitokea Ziarani Mkoani
Njombe,baada ya kuikamilisha ziara yao ndefu ya Mbeya na Ruvuma katika
mikakati ya kukiimarisha chama chao.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana Dkt.Asha-Rose Migiro Nape Nnauye wakishuka
kwenye treni mara baada ya kusimama kwa muda katika kituo cha
Mlimba,mkoani Morogoro kwa ajili kuzungumza na baadhi ya Wananchi.
Treni ya TAZARA ikishusha na kupakia abiria kituo cha Mlimba,Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...