Kivuko kikubbwa cha MV Magogoni leo kimekwama katikati ya bahari katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na hitilafu za kiufundi.Pantoni hilo linafanya safari kati ya Kigamboni na Magogoni, Dar es Salaam. Kiini cha kizaazaa hicho bado hakijafahamika, ila mashuhuda wanasema  Kivuko kilipoteza mwelekeo majini  kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya kazi. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hilo ni funzo kwa watu wa temesa kwa kivuko kutembea kwa engine mbili au moja badala ya nne kwa tabia zao za kubana mafuta na kuyauza.Kama panton limetengenezwa kwa engine nne wao wanalitembeza kwa engine mbili kwanini lisipate itirafu. Wizi Mtupuuuu.

    ReplyDelete
  2. Haya umuhimu wa kujua kuogelea unahusika hapo! nashauri waakzi wanaovuka maji kuanza kujifunza kuogelea kwa wasiofahamu. Maana kuzungukwa na maji sio mchezo, hivi wanakuwa na maboya kwenye pantone au...? Mungu iponye Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  3. Serikali inapaswa kusimamia vema mamlaka ya vivuko pasipo kulegalega.Lisemwalo na na.1 sio la kupuuzia.Huu ni mwisho wa mwaka;isije kutokea majanga kutokana na ulegelege katika usimamiaji.Ni lazima tubadilike!

    ReplyDelete
  4. Msemaji na. 1 namuunga mkono na kuongeza kuwa, Serikali iangalie pia makusanyo yatokanayo na vivuko hivyo kununua vivuko vingine vikubwa 2 kwani bila ya kuwa mchumi hebu kaa pembeni ya gati uone magari yavushwayo na watu wavukao kwa siku nadhani si chini ya 14 milioni zinazokusanywa. Hii Big Result Now (BRN) isielekeze nguvu zake kwenye barabara tu wafanye maboresho kwenye vivuko, Serikali isingojee majanga ndio wanunue vivuko vipya. Kivuko cha Magogoni kinatoa moshi kama garimoshi la zamani kuonyesha ubovu wake pia ni athari ya kiafya kwa wananchi wavukao. Serikai iwapime wananchi wa Kigamboni itawakuta wengi wana matatizo kwenye mapafu kutokana na moshi mbaya. Naomba pia TEMESA wamuweke mfanyakazi 1 atakayehakikisha magari yakiwa ndani ya kivuko yanazimwa kwani nayo yanatoa moshi mbaya kwa afya ya abiria. Sijui Mh. Magufuli anataka tuogelee kama alivyokwisha sema????? Mhe. huyu kaelekeza nguvu zake zote kwenye barabara hii ni sawa Mhe Rais ?????. Mbunge wa Kigamboni unasema nini kuhusu mapato yatokanayo na vivuko kurudisha huduma za vivuko?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...