Na Andrew Chale,Zanzibar
MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin amepata pigo kufuatia kufiwa na kaka yake, Aliyefahamika kwa jina la Athuman Bakari, Msiba uliotokea Kisiwa Ndui, Unguja.
Akizungumza kwa majonzi, Asia Idarous alisema kuwa, kuondokewa na kaka yake huyo ni pigo kubwa kwao na kumuombea.
“Familia ipo katika masikitiko makubwa, hivyo tunamuombea kwa Muumba” alisema Asia kwa masikitiko.
Na kuongeza kuwa, mazishi ya msiba huo yanatarajiwa kuwa mchana wa leo Desemba 31, huko huko Kisiwa Ndui, Zanzibar.
Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajiuuunnn !!!
ReplyDelete