Na Abdulaziz Video, Kilwa
Mtu mmoja aliefahamika kwa Jina la Nice Mtega fundi mkuu wa Meli
ndogo ya mizigo iitwayo MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro anahofiwa kufa maji baada
ya kutoweka kwa zaidi ya masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo katika
bandari ya Kilwa masoko.
Akiongea na Globu ya Jamii hii iliyofika katika eneo hilo, meneja wa Bandari ya
Kilwa, Bw. Iddi Omary, alieleza kuwa Meli hiyo iliyofunga gati jana jioni
ikitokea songosongo na kupakia tani 30 za mchanga na tani
30 za maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo Nahodha wa Meli hiyo
Captain Charles Kalinga na wasaidizi wake 3 walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliekuwepo ndani hajaonekana hadi sasa. Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana
Meli hiyo ikiwa imezama majini katika gati la Kilwa Masoko
Sehemu ya chini ya meli
MERCI III kabla ya kuzama
Meli ikiwa majini




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...