Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Mkazi wa Bagamoyo, Asha Vitalis tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa jili ya safari ya kwenda kufanya kazi Dubai, aliyotafutiwa kazi na kampuni hiyo. Hafla hiyo ya kukabidhi tiketi kwa Watanzania wawili walioondoka kwenda kufanya kazi Dubai, ilifanyika Dar es Salaam juzi. Mpaka sasa kampuni hiyo imewatafutia kazi ughaibuni zaidi ya Watanzania 100.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Mkazi wa Kinondoni, Neema Ndunguru tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda kufanya kazi Dubai, aliyotafutiwa na kampuni hiyo. Hafla hiyo ya kukabidhi tiketi kwa Watanzania wawili akiwemo Asha Vitalis (aliyekaa kushoto) walioondoka jana kwenda kufanya kazi Dubai, ilifanyika Dar es Salaam juzi. Mpaka sasa kampuni hiyo imewatafutia kazi ughaibuni zaidi ya Watanzania 100.
Asha na Neema wakisikiliza kwa makini wakati Mtemvu alipokuwa akizungumza nao kuhusu ajira yao hiyo
Mtemvu akiwa na Asha, Neema pamoja na baadhi ya wadhamini wao na baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Bravo.
Mtemvu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, akiwa katika picha ya pamoja na Asha (kushoto) na Neema baada ya kuwakabidhi tiketi. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Kweli ccmhhh wamepania kutoa ajira
ReplyDelete