Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amehimiza Waingereza na Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kuongeza kiwango cha uwekeza nchini ili kuchangia ukuaji wa uchumi nchini. Aliyasema hayo jana jijini London, Uingereza wakati akihutubia Mkutano wa Biashara na Uwekezaji ulioandaliwa na taasisi ya The New Deal Africa ya nchini humo.
Taasisi hiyo ilishirikiana na Ubalozi wa Tanzania, Kituo cha Biashara cha Tanzania na Kituo cha Biashara na Uwekezaji cha Uingereza (UKTI) kufanikisha mkutano huo.
Balozi Peter Kallaghe akimkabidhi tuzo la amani na uongozi bora Mheshimiwa Fredrick Sumaye.
(TCRA imepewa Award ya Taasisi Inayoboresha Maisha ya Watanzania kwa huduma kwa jamii kwa kusimamia sekta ya Mawasiliano.) Ndugu innocent Mungy akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya TCRA na Mh. Sumaye alisema ni matumaini yake kwamba ikiwa Watanzania hao na serikali ya Tanzania, watatumia matokeo ya mkutano huo ipasavyo, watashiriki na kuchangia ukuaji wa pato la taifa. “Ni matumaini yangu kuwa matokeo ya mkutano huu yataongeza miradi ya uwekezaji Tanzania kutoka kwa wawekezaji wa Uingerezana raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi,” alisema.


.png)
.png)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...