Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akisisitiza jambo alipo kuwa akiongea na Uongozi wa ngazi mbali mbali za Mkoa na baadhi ya vijana wa mkoa wa Dodoma waliokabidhiwa heka 50 za mashamba ya ushirika.
Mkuu wa Mkuu wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bibi Rechal Chuwa, Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa na Mkuu wa Magereza Wilaya ya Bahi Bw; Ramadhani H. Mabere wakiwa wameshika zana zao za kazi tayari kusaidiana na vijana zaidi ya 100 kusafisha shamba lenye heka 50 la vijana hao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akimsikiliza kwa Makini alie kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bahi Bw Sustenance Mpandu alipo amua kuachana rasmi na Chama chake na kuungana na vijana wapenda maendeleo wa Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi alie vaa sare ya timu ya Taifa katikati na kulia kwakwe ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty C. Mkwasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mbali mbali pamoja na baadhi ya vijana wapenda maendeleo wa Mkoa wa Dodoma wakiinua zana zao za kilimo juu kuashiria kuwa Uhuru ni Kazi. picha na Madau Sixmund J. Begashe

Vijana nchini wametakiwa kuacha tabia ya kutumika na kutumia nguvu na akili zao kwa manufaa ya wachache bali wazitumie kwa manufaa yao na ya Taifa kwa ujumla kama ishara sahihi ya ukombozi wa vijana kifikra na kutambua kuwa Uhuru ni Kazi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi katika maadhimisho ya aina yake ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania kimkoa yaliyo fanyika wilayani Bahi, Dr Nchimbi aliwapongeza vijana hao zaidi ya mia moja walio jikomboa kifikra kutoka vyuo vikuu, wahitimu na waendesha Boda Boda wa Mkoani hapa kwa kufanya maamuzi ya busara na kuondokana na fikra potofu za ajira bora ni ile ya kuajiriwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...