Mkurugenzi mkuu wa PSPF Bwn. Adam Mayingu akiuza sera za PSPF alipokutana na wanaDMV Jumapili Dec 8, 2013. Pamoja na kuanguka kwa theluji DMV Watanzania walijitahidi kutokea kwenye mkutano huo na baada ya mkurugenzi mkuu kumaliza kumwaga sera kulikua na kipindi cha maswali na majibu. Skiliza sera za PSPF hapa chini kama zilivyoelezwa na Mkurugenzi Mkuu huyo.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly akitambulisha viongozi wenzake kwa PSPF na kuutambulisha msafara mzima wa PSPF kwa wanaDMV.
Meneja wa mawasiliano, masoko na uenezi wa PSPF Bi. Costantina Martin akifafanua moja ya swali lililoulizwa na mmoja ya Watanzania wa DMV waliofika kwenye mkutano huo.
Meza kuu kutoka kushoto ni Grace Mgaza ambaye ni mjumbe wa bodi ya udhamini  wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Meneja mawasiliano, masoko na uenezi wa PSPF Bi. Costantina Martin, Rais wa Jumuiya DMV, Iddi Sandaly, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bwn. Adam Mayingu, Kaimu deski la Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Bi.Rosemery Jairo na Mama Kimolo.
Mwakilishi wa PSPF mlimbwende wa kimataifa Flaviana Matata (kushoto) akifuatilia mkutano huo wengine katika picha ni Magie na DMK.
Juu na chini ni Watanzania wa DMV waliohudhuria mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...