Muigizaji wa vichekesho kwenye kundi la Mizengwe Hemedi Khalida maarufu kama Mkwere ameangukiwa na neema ya ubalozi wa kuhamasisha upatikanaji wa jina la kampuni ya simu iliyoziduliwa bila jina. Kampeni hiyo itafanyika kupitia simu na mitandao mbalimbali ambapo wananchi wanatakiwa kuipatia jina kampuni hiyo. Mbali na hayo Mkwere atapata nafasi ya kupita mitaa mbalimbali akiwahimiza wananchi kupiga kura.
Sekta ya mawasiliano ya simu Tanzania na Afrika Mashariki imepata matumaini mapya kufuatia kuingia kwa kampuni mpya ya simu ya kipekee, ya ubunifu, yenye kuamini jamii, na yenye ushindani kuliko zote, kuzinduliwa bila jina.
Pamoja na ahadi yake ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya mtandao wa simu, kampuni hiyo mpya kwa wakati mmoja imezindua pia kampeni ya kiubunifu inayotambulika kwa jina la “Tupe Jina” itakayofanyika kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi katika simu kwa lengo la kuipa fursa Afrika Mashariki kuichagulia jina bora kampuni hii kwa kupiga kura.
.jpg)
Hii ni kampuni ya kwanza ya simu Afrika Mashariki ambayo kweli inajali na haigopi kuamini watu, na hakuna kampuni nyingine inaweza kuthubutu kufanya hivyo. Hakuna kampuni yoyote duniani iliyoweza kuzinduliwa bila jina na kutoa jukwaa kwa kampeni ya kusisimua kabla ya jina kuwekwa hadharani.
“Tupe Jina” ni kampeni itafanyika kwa awamu mbili katika mtandao, ujumbe wa simu na mtandao wa kijamii wa facebook. Katika awamu ya kwanza, Afrika Mashariki inapaswa kuteua majina ambayo wanapenda hii kampuni mpya iitwe.
Mshirki anaweza kuchagua jina kwa kuingia katika mtandao wa Unaweza kuteua jina kwa njia ya magogo kwenye mtandao wa www.giveusaname.net au kutuma ujumbe wa simu ukiambatanishwa na jina analopendekeza kwenda namba 15678 au aingie katika mtandao wa www.facebook.com/giveusaname. Katika awamu ya pili ya kampeni, jopo litatathmini majina yote na itatoa majina matano ambayo yamependekezwa mara nyingi zaidi, ya kipekee na yenye ubunifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...