Mkurugenzi wa Msama Promotions,Inayoandaa tamasha la Krismasi,Bwa.Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa msimamizi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi,Haruna Mtandika.

Hafla hiyo ilifanyika hapo jana kwenye ofisi za kampuni hiyo jijini dar,vituo vitano vilinufaika na msaada huo ambavyo ni onorata Temeke,Mwandaliwa Boko,Malaika Kinondoni,Yatima Group Truts Fund ya Chamazi na Mahabusu ya Watoto Upanga,vyote vya jijini Dar.Makabidhiano yao yamefanyika jana kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo Kinondoni jijini Dar.
 Baadhi ya Wanahabari mbalimbali waliofika kwenye tukio la Msama Promotions Ltd,ilipokuwa ikikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuuu za Krisimasi na Mwaka mpya kwa vituo vitano vya Watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu,jijini dar jana. 
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Inayoandaa tamasha la Krismasi linalotarajiwa kufanyika kesho Duniani kote,Bwa.Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha Mwandaliwa-Boko jijini Dar,Bi.Halima Mpeta.

Mwenyekiti wa Tamasha hilo Bwa.Msama amesema kuwa kama ilivyo ada ya kampuni yake,imeamua kutoa kiasi fulani cha mapato yake ya tamasha hilo na kununua vyakula kwa ajili ya kuwapa zawadi watoto yatima na wasiojiweza ili na wao washerehekee sikukuu kwa furaha kama wenzao.

Vituo vilivyopata zawadi hizo ni Honorata Temeke,Mwandaliwa Boko,Malaika Kinondoni,Yatima Group Truts Fund ya Chamazi na Mahabusu ya Watoto Upanga,vyote vya jijini Dar.Makabidhiano yao yamefanyika jana kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo Kinondoni jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...