MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli ndani ya chama.
Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza
Maamuzi na vitendo vinavyoendelea ndani ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa demokrasia ya kweli tunayoihubiri mbele ya umma.
Kwa barua hii basi, nimeonelea bora upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na dhamira yangu inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.
Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu tayari.
Ninatanguliza shukrani zangu za dhati kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati kuu ya chama.
Kusimamia haki, katiba na misingi ya chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba macho pindi ujinga wa namna hii unapoendelea kutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.
Nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako.
………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu
MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
YAMETIMIA MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHO YANGU
ReplyDeletehayo ni maoni yako. hizo sababu umezigundua lini? nenda wakokuita babu.
ReplyDeleteKila mtu atajifanya Zitto Kabwe.Acheni unafki kwenye Siasa.
ReplyDeleteJua linazidi kuwawakia wabakaji wa chadema. wakuu jiuzuruni kukinusuru chama
ReplyDeleteNi mh Raisi kikwete tu anaweza kukaa moja moja na watu wanaotofautiana. Hicho chama kinachoongozwa na wavimba nyuso kila wakati smile kwao mwiko sidhani kama wanaweza kuazima busara za kurejea maamuzi yao.Zitto ni mtu wa taifa na si chama.
ReplyDeleteNimeipenda hii
ReplyDelete"Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mapaka hapo mtakapopata anuani yenu tayari"
Daaah CHADEMA kweli hamna anuani ya posta hadi mnatumia anuani ya mtu binafsi.
Chadema fanyeni pangua pangua yenu lakini chonde chonde kama tunavyo tunavyo wafahamu ninyi kama Mdau wa 5 anavyosema kuwaita 'wavimba nyuso' kamwe MSIBEBE MAPANGA, HALAFU MKAKATANA MASIKIO NA MIKONO KAWOSHI!
ReplyDelete