Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Barabara bado si user friendly kabisa. Me sizielewi kabisaaa. Hasa kwenye makutano..hivi kwa nini mnaohusika mhe. Waziri jengeni makutani nyingine ipite juu na nyingine chini ili kusiwe na usumbufu wa matrafiki kukaa kwenye makutani hayo au umeme unapokatika. Mfano makutano ya Ubungo, magomeni, Morocco, fire, akiba, bibi titi yote, karume, chang'ombe..hivi mnawashirikisha kweli wadau ktk ujenzi huu? Kwa mtazamo wangu kazi bado iko kubwa mno.

    ReplyDelete
  2. kwa mpango huo bado kabisa maana mabus yaendayo kasi nabidid barara iwe clear kuepuka ajali lakini hii sivyo waendendsha baiskeli, waenda kwa miguu hamjawafikiria sasa waktiza hovyo na hayo mabus itakuwaje fanyeni kitu kinachoeleweka sio kifanya mradi kama kichwa cha mwendawazimu

    ReplyDelete
  3. Hata mimi sizielewi kama mdau hapo juu uliyoandika! Labda tusubirie wakimaliza kabisa, au isisje kuwa hapo ndio wamemaliza nini!! Mungu ibariki Tz na watu wake.

    ReplyDelete
  4. Dar kwa kweli imebadilika ukiangalia Dar ya miaka ya tisini na dar ya siku hizi kumejengeka kweli.

    ReplyDelete
  5. Michuzi
    Huoni kuwa ingekuwa bora haya mabasi yaendayo kasi yangeitwa mabasi ekspresi,ni kuazima lugha, siku zote twaazima lugha.Inaposemwa mabasi yaendayo kasi, naingiwa na hofu kidogo kuwa mabasi hayo ni hatari.

    ReplyDelete
  6. Mabadiliko makubwa sana nilikuwepo mitaa hii miezi minne iliyopita walikuwa bado wapo kazini ukweli wamefanyika vizuri.
    Mdau 1-1 sifahamu unaishi wapi kwa mabadiliko kama haya tunawajibika kuwasifu wahusika tusijifananishe
    na nchi zilizoendelea tunajipanga.
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  7. Hiyo ni barabara ya mabasi hayo tu.so hizo ajali mnazozungumzia zitatoka wapi.tatizo wengi wenu mnaona Tanzania watu wote hawana akili.
    Maendeleo ni makubwa waliojituma wanastaili pongezi sana.
    Subirini mwisho wake mtaelewa.hiyo ni kama mathematics ambayo najua wengi wenu mlioponda mlifeli kama sio kukimbia.
    Bongo inanoga mbaya.

    ReplyDelete
  8. Miradi kama hii kwaasili yake huwa ni endelevu na wakati wote nafasi ya maboresho ipo....japokuwa ikiwa zipo kasoro za msingi ni lazima zifanyiwe kazi mapema na kwa maana hiyo mawazo ya wadau mbalimbali wa usafiri & usafirishaji mijini ni muhimu yakasikilizwa na inapowezekana yaweze kufanyiwa kazi.

    Lakini na sisi "wadauz" wajemeni nadhani ni vizuri tujifunzage kujenga utamaduni wa kuwapongeza watendaji wa serikali .... maana tukifanyahivyo na sisi tutakuwa tumetoa mchango wetu ili kukifanya hicho kilicho chetu kiwe bora zaidi kwa ustawi wa jiji letu la Dar na miji mingine ikiwa mradi huu pia utamudu kujipambanua kwa ustawi wa miji mingine katika hii TZ yetu.

    ReplyDelete
  9. Barabara za Mabasi yaendayo Kasi:

    Changamoto mbili (2) nizionazo mimi Mdau ni kuwa

    (1.)Ule Utamaduni wetu wa maisha pale Magomeni Mapipa ambapo mimi ninaishi upande wa pili wa barabara wakati kila siku VITUMBUA VYA KUNYWEA CHAI ASUBUHI nachukua kwa mama Bahati upande wa pili wa barabara!,,,MFANO NIMEAMKA NA TAULO YANGU KIUNONI NA FLANA YA SINGILETI NINAJIANDAA KUVUKA BARABARA NIKACHUKUE VITUMBUA NA HUKU BASI LIENDALO KASI LIKIELEKEA MJINI LIMEACHIWA SPIDI MOTO CHINI KUTOKEA UBUNGO!,,,WANDUGU WA MPANGO WA MABASI YAENDAYO KASI MTANIBEBA VIPI HAPO MIMI NA MAZOEA YA MAISHA YANGU YA MAGOMENI?

    2.Ile tu mabasi yetu ya kawaida ya Toyota-DCM (YASIYO YA MWENDO KASI) usalama wetu haupo kamili JE MABASI YAENDAYO KASI ITAKUWAJE ? WAKATI KAMA WANAVYO SEMA WADAU HAPO JUU KTK BARABARA HAKUNA HIZO FLY OVERS ZA VIVUKO?

    ReplyDelete
  10. Jamani tusijidhiki kiasi cha kukubali kitu hata kama ni kibaya, kikiwa kibaya kisemwe wahusika wapate kujirekebisha, nchi Tanzania inaweza sana kama viongozi watakua waaminifu. Barabara ndio maendeleo ya nchi hivyo basi itengenzwe kwa kiwango kinacho kubalika, mitaro iwekwe mifuniko kuwe na vivuko wenda kwa miguu na baiskeli pia wafikiriwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...