Bi. Shida Mapele akiwa hospitalini kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya na mchumba wake.

Na Abdulaziz Video

Huku Dunia ikiwa Imeazimisha Siku 16 za harakati dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,huko Wilayani Liwale Mkoani Lindi, Mkazi Mmoja wa kijiji cha Naluleo aliefahamika kwa Jina la Shida Mapele amejeruhiwa vibaya kwa Mapanga na Mchumba wake na kumsababishia ulemavu wa kudumu baada ya kumkata mkono wa kulia na kumjeruhi katika baadhi ya viungo vyake.

Hii ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu na uvunjaji wa haki za binadamu licha ya Mtuhumiwa kufikishwa mbele ya Sheria,Wanawake wilayani Humo wametakiwa kutetea haki zao huku wakiomba sheria ichukue mkondo wake dhidi ya ukatili huo uliofanywa na Bw. Ally Burian ambae anashiliwa na Jeshi la Polisi.

Akiongea na Ripota wa Globu ya Jamii Wilayani humo,Mratibu wa Asasi ya kutetea wanawake na watoto(Liwopac)Bi Hidaya Chikawe alieleza kuwa licha ya harakati zinazofanywa na wanawake kuelimisha jamii Bado Vitendo hivyo vinashika kasi wilayani humo.

“Hakika kwa tukio hili ni Ishara tosha inayodhihirisha kuwepo kwa ukatili wilayani humu,Hapo Awali tulizoea kusikia katika mikoa ya wenzetu lakini sasa Dunia imebadilika tunashuhudia matukio haya mara kwa mara”alieleza Chikawe.

Aidha aliwataka akina mama wa liwale kuanza kujitetea kwa kufichua uhalifu unaojitokeza kutokana na Takwimu ya mwaka jana inaonyesha matukio hayo kuwepo kwa 2% lakini sasa hali inaongezeka kila mara hususan kipindi hiki cha mauzo ya korosho.

Kwa Upande wao baadhi ya akinamama walisema licha ya historia ya matukio mabaya kutokea wilayani humo tukio hili la kumsababishia ulemavu mwanamke huyo kutokana na kukatwa kwa mapanga.

Walieleza walivyoguswa na tukio hilo huku wakitoa wito kwa jamii na serikali kuchukua hatua kali kwa wahusika wanaobanika na kukamatwa.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ambapo hivi karibu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi wa Polisi Bi Renatha Mzinga alianzisha kampeni ya kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na matukio hayo katika maadhimisho ya siku 16 za ukatili dhidi ya Mwanamke ambapo walifanikisha kutoa misaada na usafi katika kambi ya wazee na walemavu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Cha msingi Masheikh wasaidiwe wapeleke elimu ya maadili huko vijijini kwa kuwa watatoa mwongozo uliokuwa sahihi kulingana na Yule aliyetuumba, wewe na miye na viumbe vyenginevyo, n.k.

    ReplyDelete
  2. Wazazi, acheni kabisa kuwapa watoto wenu wazuri majina ya "SHIDA".

    ReplyDelete
  3. Mbona haya mambo yamekuwa mengi mno, sheria iko wapi? Kama sikosei, nimesoma matukio manne sasa mwaka huu.

    ReplyDelete
  4. Inauma sana, but na upande mwingine wa shilingi uangaliwe!

    ReplyDelete
  5. Hivi haya mambo yalikuwa toka zamani na sasa tunayasikia sababu ya technology au mapya? Kwa kweli inasikitisha sana. Serikali inabidi kuwaelimisha watu kuwa binadamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...