Okwi akilakiwa kwa shangwe na mashabiki waliofika kumpokea mapema leo jioni.
 Okwi akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Yanga waliofika uwanja wa ndege kumpokea  leo jioni jijini Dar es salaam
 Okwi akionesha namba yake ya mashambulizi siku ya jumamosi

HATIMAYE mshambuliaji raia wa Uganda Emanuel Okwi ametua nchini leo majira ya saa tisa na nusu alasiri  na kupokelewa na viongozi wa Yanga katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Okwi  ambaye amesajiliwa Yanga kwa miaka miwili na nusu kwa jumla ya dola 60,000 alitua nchini na ndege ya  shirika la Rwanda.
Mbali na viongozi hao wa Yanga ambao ni Abdallah Binkleb, Musa Katabalo na Seif Ahmed  'Magari' pia alilakiwa na wanachama wachache ambao walijitokeza uwanjani hapo kwa lengo la kushuhudia ujio  wake.

Akizungumza mara baada ya kutua uwanjani hapo Okwi ambaye amezaliwa  Desemba 25, mwaka 1992  alisajiliwa Simba akitokea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la  dola za Kimarekani 40,000 alisema "Mimi ni mchezaji na mpira ni kazi yangu, nimekuja kuichezea Yanga na  nitaitumikia kwa mapenzi yangu yote, nimekuja kufanya kazi na si kuiangalia Simba, mkataba wangu na Simba  ulishaishaga.

Akizungumzia mechi ya Yanga na Simba itakayofanyika Jumamosi ijayo alisema "Mimi nipo fiti, nipo tayari  kucheza mechi ya Simba, nimejiandaa kikamilifu, ila mwenye maamuzi ya mwisho ya mimi kucheza au  kutocheza ni kocha, kama atanipanga nitafurahi zaidi."alisema Okwi ambaye amejiunga kambini na wenzake jana  jioni kwenye hotel ya Protea iliyopo Oyesterbay jijjini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya  Nani Mtani Jembe Jumamosi.

Kuhusu utata wa usajili wake Yanga, Okwi alisema "Mimi hayo mambo siyajui, nimeyaacha mikononi mwa  viongozi wa Yanga ndio watakaomaliza hilo suala."alisema Okwi ambaye baada ya mkataba wake na Simba  kuisha Desemba mwaka jana aliongezewa mkataba wa miaka miwili na Simba kabla hajaanza kuutumikia  akahamia Etoile du Sahel ya Tunisia ambako aliuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 fedha ambazo Simba  wanazisotea  mpaka leo kwa kile walichoeleza kuwa Etoile haijawalipa.

Kufuatia hali hiyo, Simba walipeleka malalamiko yao Fifa kuishtaki Etoile ambayo nayo ilipeleka malalamiko  ya Okwi kuwa ametoroka kwenye klabu hiyo, ambayo hata hivyo alidai alikalishwa benchi miezi mitatu bila  kuchezeshwa wala kulipwa mshahara wake kitu ambacho kilimfanya atimkia nchini kwao Uganda miezi  michache iliyopita na Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), lilimuombea kibali mchezaji huyo Fifa ili ajiunge  na klabu ya Sports Clab Villa ili kulinda kiwango chake na Fifa ilimuidhinisha kuichezea klabu hiyo kwa muda   wa miezi sita suala lake likiwa linashugulikiwa na tayari ameichezea klabu hiyo kwa  miezi miwili.

Tayari Fufa wameiandikia Fifa barua kutaka ufafanuzi  wa usajili wa mchezaji huyo Yanga kwa vile alizuiwa  kucheza michuano ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwa vile  hajamaliza matatizo yake na Etoile du Sahel.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb alisema "Baada ya mechi ya Jumamosi  tutatoa ufafanuzi zaizi kuhusu usajili wa Okwi, sisi hatujakurupuka, tumemsajili kwa ajili aweze kutusaidia  kwenye mechi zetu za kimataifa, tunaenda kupeperusha bendera ya Tanzania hivyo Simba wawe wazalendo,  kumsajili Okwi ni kama kunogesha 'ice' kwenye keki, tunalenga kuhakikisha michuano ya klabu bingwa mwakani tunafika mbali.

Kauli ya Binkleb imekuja kukiwa kwa mahasimu wao Simba kunawaka moto kwa wanachama kumshinikiza  mwenyekiti wao Ismail Aden Rage kujiuzulu huku wakimtuhumu kutafuna dola laki tatu za mauzo ya Okwi kitu  ambacho Rage anakipinga vikali kwa kusema hajatafuna fedha hizo na kuweka ngumu kujiuzulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...