Waziri wa Maji,Prof. Jumanne Maghembe hivi karibuni alifanya ziara ya kushtukiza ili kuangalia maendeleo yaliyofikiwa na Wahandisi wanaoandaa ujenzi wa miundombinu ya maji katika Tank la Maji la Muhalo, Tarafa ya Mashimba(Shinyanga Vijjijini) kwenda Ngudu, Wilaya ya Kwimba.

 Aidha, Waziri aliangalia michoro itokanayo na usanifu wa mradi huo ambao unatarajiwa kugharimu Shs. 2.8 bilioni.

Wataalamu wanaosimamia ujenzi huo sasa wanapokea zabuni za utengenezaji wa mabomba yatakayo tumika kutoa Maji Mhalo hadi Ngudu. Katika ujenzi huo vijiji 7 vilivyoko njiani kati ya mhalo na Ngudu navyo vitafaidika na mradi huu. Mradi huu utakao tekelezwa katika kipindi cha miezi 6.
Waziri wa Maji,Prof. Jumanne Maghembe akikagua Tank la Maji la Muhalo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. anakagua maji au anakagua ngazi kama ipo imara? mbona anaogopa kumalizia kupanda ngazi?

    ReplyDelete
  2. Mi nafikiri maelezo ya Picha yasomeke Prof. Magembe akiwa amekula pozi la kupigwa picha...

    ReplyDelete
  3. Konoz magembe, daah uko juu kama sanamu mpya ya mandela!

    ReplyDelete
  4. Mnaniona? nani anasema mi waziri mzigo

    ReplyDelete
  5. Anonymous Anonymous said....
    Hahahahahaha! Mdau wa kwanza na wa pili nahisi mpo sahihi kabisa. Kugagua maji si kazi rahisi bwana.

    ReplyDelete
  6. Mimi nafikiri anakagua ukuta. kama mawe yamepangwa vizuri.

    ReplyDelete
  7. Naona waziri ajitahidi kufuata health and safety regulations at work kwani yeye ni kioo cha taifa.

    ReplyDelete
  8. tumekusoma muuza sura.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...