Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati aliposimama kwa muda katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano unaohusu Amani na usalama na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Bara la Africa na Ufaransa.Kulia aliyesimama ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed na kushoto ni afisa itifaki.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed wakati aliposimama kwa muda katika uwanja wa ndege jijini Nairobi, Kenya alipokuwa akirejea nyumbani akitokea Paris Ufaransa ambapo alihudhuria Mkutano uliohusu Amani,Usalama na Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na bara la Afrika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Mec Sadik akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi baada y kuwasili akitokea Paris Ufaransa ambapo alihudhuria Mkutano wa Amani,Usalama na Ushirikianokati ya Afrika na Ufaransa uliomalizika jana.(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ktk Kundi la CoW 'Coalition of the willing' angalau Kenya wana mwelekeo wa Kismati na Kistaarabu!

    Baada ya Raisi Kikwete kutoa Hotuba yenye ukweli uliosheheni Kenya ilitoa Tamko kuunga mkoni Msimamo huo kitu ambacho walionyesha wao wanamwamko sana kiuelewa kuliko Kampla na Kigali.

    Ni kuwa Kampala na Kigali walikaa kimya kwa kuwa wao ni viburi wakati Kimataifa hawauziki kabisa kwa sasa!, si UN, si Marekani, si Ulaya si China!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...