Kama tulivyotoa taarifa kwa vyombo vya habari hapo awali   wakati wa Sikukuu ya Noel (Christmass) Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa, baada ya kujumuika na watoto waishio katika mazingira magumu kule Bigwa Morogoro katika Kituo cha Mgolole,

Mrembo huyo ataungana na warembo wengine watatu, akiwemo Miss Tanzania mshindi wa pili Latifa Mohamed, Miss Tanzania mshindi wa tatu   Clara Bayo, kukabidhi misaada ya kijamii pamoja na kushereheka nao pamoja wakati wa Sikukuu ya Mwaka mpya tarehe 1 Januari 2014, katika kituo kiitwacho Nira Children and Youth Orphans Foundation kilichopo eneo la Mbagala Nzasa A, kwa mzungu kaburi moja, Kata ya Charambe, Wilaya ya Temeke.

Miss Tanzania pamoja na warembo wenzake, watakabidhi misaada hiyo ya vyakula, ikiwa ni pamoja na vifaa vya shule, kama vile Madaftari, kalamu,  vitabu n.k.


Wakati huo huo Mrembo wa Kanda ya Mashariki Diana Laizer, kutoka Mkoa wa Morogoro, nae atakabidhi misaada kama hiyo katika Kituo cha Amani kilichopo Manispaa ya Morogoro, pamaja na kushereheka nao katika Sikukuu hii ya Mwaka mpya 2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...