Kwa Niaba ya CCM Tawi la Uingereza tunapenda kuungana na Wanachama, Wapenzi na waTanzania wote kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu za Krismas na Ujio wa Mwaka Mpya wa 2014.

Uingereza sherehe hizi zimetukuta katika hali ya hewa yenye kimbunga kingi na mvua nyingi zisizoisha, na hivyo kuathiri maandalizi kwa namna moja au nyingine kutokana na vizuizi katika baadhi ya miundo mbinu hasa barabara na reli.

Aidha, kama inavyojulikana Ulimwenguni Ukata wa kifedha nao umeshika hatamu. Kuyumba kwa Uchumi wa Nchi nyingi kubwa na ndogo na kuyumba kumepelekea mfumuko wa bei za bidhaa hasa vyakula . Tatizo ambalo limeukumba ulimwengu mzima.

Licha ya vikwazo hivi na vingine ,hatuna budi kumaliza mwaka kwa kuangalia nyuma na kuona yale mengi yaliyofanikishwa. Kwa hali hii , CCM UK tunachukua nafasi hii kuipongeza kwa dhati Serikali ya awamu ya nne ya Jamahuri ya Muungano ya Tanzania kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.

Mfano ulio wazi ni katika miundo mbinu ya barabara ambapo asilimia kubwa ya Nchi sasa inaunganika kwa barabara na maeneo mengi sasa yanafikika kirahisi kwa barabara,ambazo nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami. Hii imesaidia sana kupeleka mahitaji muhimu vjijini na uvutiaji katika uwekezaji, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Tunapenda kuwasihi WaTanzania wenzetu , tutumie kipindi hiki cha mapumziko ni vyema pia kutafakari na kupongeza yale mazuri yaliyofanywa na serikali na vilevile kuungana pamoja na kuchangia katika kuleta Maendeleo ya Mtanzania na si kubeza juhudi za maendeleo kwa sababu ya tofauti za kiitikadi na za kisiasa .

Ni muhimu kwanza tujipongeze wenyewe kama watanzania kwa nafasi pekee tuliyonayo na tunayojivunia ya amani ya nchi yetu. Tusikubali kurubuniwa kwa namna au hali ya aina yeyote na hasa inapobidi tujiulize na kutafakari ni nini kinatufanya watanzania tukawa wamoja , vilevile kudumisha Amani, Umoja na Upendo wetu.

WaTanzania hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu na upendo miongoni mwetu kwa gharama yeyote ile na bila kuyumbishwa au kutetereka ili tuweze kuachia vizazi vyetu vijavyo Urithi ulio mwema kuliko wowote Ule. TANZANIA yenye Amani, Upendo na Utulivu.

"MUNGU IBARIKI TANZANIA"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...