KOCHA wa Sakatari,Innocent Mathew ameiomba Serikali kuanzisha Chuo cha mafunzo ya mchezo huo ili kutoa nafasi kwa vijana wa kitanzania kupata ujuzi utakaofanikisha kujiajiri wenyewe.

Akizungumza Dar es Salaam leo na waandishi wa habari, alisema Tanzania ina vijana wengi wenye vipaji katika michezo mbalimbali ila kinachowakwamisha ni kutokuwa na sehemu ya kuwaendelea ili kuwa na ufanisi mkubwa utakaoendana na ushindani kimataifa.

Mathew ni miongoni mwa vijana 12 wanaounda kundi la Hakuna Matata ambalo linafanya shughuli za maonesho ya sanaa za jukwaani, ikiwemo uigizaji na Sarakasi katika visiwa vya Macau pamoja na nchi ya China, alifafanua kuwa ikiwa Serikali na wadau wa michezo watafanya hivyo itasaidia vijana wengi kupata fursa ya kujifunza na kuondokana na kuikaa vijiweni.

"Naamini ikiwa Serikali na wadau wa michezo watatoa hudumu hiyo kwa kuwajengea vijana vyuo vya aina hiyo itafanya kuwapa fursa ya kujitengenezea ajira mara baada ya kuhitimu mafunzo yao kwa kuna soko kubwa la mchezo huo nje ya nchi," alisema.

Alisema mfmno unaoweza kutumia ni kwa kutumia kundi lao ambalo lilianzishwa mwaka 2000 na tangu mwaka 2003 walinza kusafiri katika nchi mbalimbali kama vile Ujerumani, Australia,Seoul Korea,Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi, Korea Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu na baadae kutua huko Macau, China.

"Kama Tanzania inahitaji vijana wake wapate fursa ya kuondokana na umasikini ni vema ikawatengenezea fursa hiyo ili kufukia mafanikio katika malengo ya milenia mwaka 2015," alisema.

Mathew hivi karibuni alirejea nchini kwa ajili ya mapumziko akitokea China alikokuwa katika mafunzo mbalimbali ya mchezo huo, amewaomba wadau wa mchezo huo kujitokeza kumpa sapoti ili kufikia malengo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kocha wa sakatari.....mbwembwe nyingi mpaka mnachapia.Ila ujumbe umewafikia wahusika.

    ReplyDelete
  2. kwani chuo cha sanaa Bagamoyo kimeishia wapi? Badala ya kujenga kipya si kile kipanuliwe na kuongezewa ufanisi? Au kila mtu ni mwendo wa kuropoka tu?

    ReplyDelete
  3. KIKUNDI CHA SARAKASI KILIKUWA NA MAKAZI YAKE UWANJA WA TAIFA MIAKA YA SABINI BAADA YA KURUDI TOKA CHINA AMBAKO WALIPATIWA MAFUNZO, LAKINI KAMA KAWAIDA YETU KILA KITU NI CHA KUPITA TU.

    ReplyDelete
  4. Daa si mchezo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...