Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo na familia zao wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa NBC kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa NBC wakichuana katika mchezo wa soka ili kumpata mshindi katika hafla hiyo leo.
Hapa wakionyesha umahiri wa kucheza mpira wa kikapu katika sherehe hizo jijini humo leo.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara wakifurahia kuogelea ndani ya bwawa la kuogelea katika hoteli hjiyo jijini Dar es Salaam leo.
Kulikuwa na aina mbalimbali za vyakula kukidhi haja ya kila mmoja aliyehudhuria sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa NBC jijini Dar es Salaam leo.
Manahodha’ wa timu za michezo za benki hiyo wakionyesha umahiri wao kusakata rumba katika hafla iliyowakutanisha wafanyakazi na familia zao jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tanzania kweli tumetoka mbali, kizazi hiki ni cha kula kuku tu hamna matatizo mengi ya chakula mijini, miaka ya nyuma kidogo watu walikuwa wanakula kwa madaftari na chakula kilikuwa kwa foleni. Ee Mungu ibariki nchi yetu.

    ReplyDelete
  2. Ubarikiwe sana mdau No. 1-1 hapo juu, unajua kadiri tunavyoitakia nchi yetu kubarikiwa MUNGU atazidi kuibariki tu....MUNGU siyo dharimu kabisa.

    Kinachotupa msukumo wa kuitakia nchi yetu kubarikiwa ni kwavile hayo tuyaonayo sasa zamani hayakuwepo...na hii inatosha tukamshukuru MUNGU na kuzidi kuliombea baraka Taifa letu....Eee MUNGU ibariki zaidi Tanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...