Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.


Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.

Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa 
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. The mdudu,maelezo kibaoooo end of the day UMEME BEI JUU,huduma mbovu,vijijini watu hawana umeme,kazi kwenu ndugu zangu watanzania mm nishasepa hapo zamaani kabisa huku niliko umeme 24/7 na mwendo mbele sio nyuma,poleni sn ndugu zangu,hiyo Tanesco itazameni kwa jicho la 3

    ReplyDelete
  2. Ni january ya 2013 au 2014 au tarehe zinarudi nyuma. Umakini unahitajika ndio maana kila wakati umeme unakatika kwa sababu hakuna umakini

    ReplyDelete
  3. Sasa ukisepa ndio nini badala ya kutoa ushauri unajidai nimeshasepa. Huku huna ndugu zako wanaoteseka. Mkaataa kwao mtumwa.

    ReplyDelete
  4. Hata wakiongezewa kufikia asilimia ngapi bado huduma zitakuwa mbovu.

    Shirika halitapata faida yo yote kutokana na madeni yaliyoikaba koo, na waliosababisha madeni hayo hivi sasa ndiyo wanajifanya wema sana na kutoa misaada kwa wananchi kwa wingil

    ReplyDelete
  5. Unaona sifaa eti mimi nilisha sepa kitambo!! hovyoo KJ Mkubwa

    ReplyDelete
  6. hii ina maana mwenye uwezo ndio atumie umeme as if ni luxury sio muhimu, sasa jamani hii nchi ina kwenda wapi? Hayo ndio maendeleo umasikini mpaka mwisho wa dunia. Mungu saidia waja wako hasa africa

    ReplyDelete
  7. Naomba serikari hiangalie sana swala. La umeme kwani kipata cha watanzania bado kipo chini ya Dola 2 pia serekari wanapiga vita ukataji wa kuni,mkaa,pia na mafuta. Ya Taa bado yapo juu lita 2000 Gesi hipo juu waka serika ndio mda walipaswa wapunguze bei ya Gesi mafuta ya Taa pamoja na umeme angarau unit moja ya umeme Tsh 100

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...