![]() |
| Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya ardhi, maliasili na mazingira Mhe. James Daud Lembeli, Mb. |
1.0 UTANGULIZI.
Mheshimiwa Spika, wakati Bunge likijadili hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo muhimu la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2013, iliyowasilishwa na Mhe. Said Nkumba, Mbunge wa Sikonge kuhusu Mgogoro kati ya Wafugaji na Wakulima, Hifadhi na Uwekezaji, Mheshimiwa Spika alitoa Uamuzi ‘Speakers Ruling’ kuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ishughulikie kazi ya kutathmini na kuangalia jinsi Mpango wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na kutekelezwa na Serikali kupitia ‘Operesheni Tokomeza’.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za Taarifa Rasmi za Bunge za tarehe 1 Novemba 2013, wakati Bunge likihitimisha Hoja ya Kuairisha Shughuli za Bunge, Mhe. Spika alitoa uamuzi ufuatao:-
…Kamati ile ya kawaida ya Maliasili itaendelea na kazi yake ya kufanya tathmini ya kuangalia jinsi mpango ule wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na ndani yake itashughulikia kama kulikuwa na uzembe ama kuna watu wanahusika katika kuondoa maisha ya watu kwa sababu za uzembe …



Ok mawaziri wameondolewa, lakini ukweli ni kuwa hii kamati haijafanya kitu chochote cha maana ili kubadili mfumo wa sasa...
ReplyDeleteHii inachangiwa sana na elimu za hawa wabunge wetu. Nimejaribu kupitia CV ya Lembeli, inasikitisha sana jukumu muhimu kama hili la kuchunguza implementation directives za Rais aliachiwa huyu jamaa ambaye hana university degree.
Ndiyo maana unaona kupwaya sana katika recommendations, na watu kama hawa ndiyo chanzo cha matatizo.
Huyu jamaa hajui alichokuwa ana-recommend. Alinishangaza sana aliposema mifugo kuranda randa huko kwenye hifadhi ni kosa la wizara ya Mifungo. Wakati muhusika ni bwana mifugo wa wilaya chini ya TAMISEMI
Anyways tunatakiwa kuwa makini na shule za wale tunaowapa majukumu ya uenyeviti wa kamati, otherwise tutakuwa hatutatui tatizo.
Nasita kusema "Lembeli did is job", nafikiri ni kati ya failures wengine tu wanaotuharibia hii nchi.
Kagasheki na Mathayo ni majembe....mfumo ndiyo tatizo, hili lilitakiwa ndiyo liwe kiini cha hii ripoti
Tunahitaji kubadilil mfumo wa polisi,sheria na kutoa ubinafsi kwa viongozi.Kipaumbele kiwe kuendeleza taifa na kila mtanzania awe na haki sawa.Tazizo ni mfumo wa rushwa ya taasisi je tuko tayari kuubadili?
ReplyDeleteInaonyesha we mdau unae mwonesha kidole huyo m/kiti una sababu zako za kibinafsi, hii riport unatakiwa uisome, na uoza kwa ujumla upo karibu kila sehemu, hao unaodai ni wenye elimu baadhi yao ndio founder wa hizo network zinazo zungumzwa kwenye hiyo riport. cha msingi serikali imeshakabidhiwa na kazi ni ku-dili na hiyo mitandao! ianzie na wizara hiyo na zingingine zikae zikijitaarisha.
ReplyDelete-mdau holland
Lazima wewe hapo juu ni muumini ama wakala wa mmoja ya hao waliotimuliwa. Unamlaumu na kumshambulia Lembeli na kutaka kumpaka kwa CV yake, ukisahau kuwa hio haikuwa Lembeli, bali kamati ya bunge ya kudumu iliyofanya hayo kwa pamoja (collectively) nayeye kama Mwenyekiti amesoma ripoti tu. Halafu kuhusu university degree wewe hapo inaonekana unayo ya kimagamu, maana kuwaza kidogo kunakushinda, unaleta chuki na ubinafsi. Basi kwa taarifa yako IMETOKA hio. Kama ulikuwa unakinga bakuli kwa mmoja wao hao jamaa umeula wa chuya!!!!
ReplyDelete'Nasita kusema "Lembeli did is job", nafikiri ni kati ya failures wengine tu wanaotuharibia hii nchi'
ReplyDeletedoh, kazi ipo - 'Basi kwa taarifa yako IMETOKA hio. Kama ulikuwa unakinga bakuli kwa mmoja wao hao jamaa umeula wa chuya!!!!'
What's a degree, I finished std 7 and I am sure if I want to get a Phd in bongoland I would get one in 6 months. Look at the Ministers everyone seems to have a Phd but it seems they would not even be able to run a chook raffle. Good on Lembeli - keep up the hard work but for sure I think the govt should provide you with some protection. Maana kuna wajinga kama huyu mdau ambao hawataki kukuone katika dunia hii maana wewe uko na wananchi siyo fisadi. Nchi inaliwa utafikiri hakuna kesho.
ReplyDeleteLook at the Ministers who resigned a few months ago, no action was taken against them. Yote tumeshasahau maana ni tabia yetu wabongo kusahau. TUKURU should be abolished, I don't see their role at all.
Wizara ya utalii inahitaji kurekebishwa na kuwa na utaratibu mpya wa kufanya kazi,kama hakuna mabadiliko hayo tutarajie wenzetu kutumia rasilimali zetu wenyewe tukiwa tumelala mchana kweupe.Wizara iwe ya utalii tu,,,maliasili peleka mazingira huko.Kisha waziri apange mpango wa kazi na kurudisha TTB kuwa idara ndani ya wizara kuliko sasa wanatumia pesa bila sababu za msingi.Tanapa wawe na kazi ya kutunza mbuga zetu sasa utakuta mtu wa TANAPA kila mwaka yuko safari kwenye maonyesho ya utalii,kazi amabyo TTB wanatakiwa kuifanya.Kisha tunatakiwa kuwa na stategy za utalii,STP,destination image,slogan nzuri na mengine mengi lakini waziri alikuwa busy na kutoa vibari vya miti,kwenye wizara ya utalii.Napenda kuwakilisha...
ReplyDeleteMdau wa utalii.....
WEWE UNAYEMSEMA LEMBELI NA ELIMU YAKE HUNA AKILI HATA KIDOGO. KUNA MAPROFESA WANGAPI NCHI HII LAKINI MICHANGO YAO KWA TAIFA NI SIFURI? MIMI NI MSOMI MWENYE DIGRII MOJA LAKINI SIJAONA TOFUTI KATI YA MIMI NA MAPROFESA.
ReplyDeleteMIMI NI MSOMI MWENYE DIGRII MOJA LAKINI SIJAONA TOFUTI KATI YA MIMI NA MAPROFESA.
ReplyDeleteFUNDAMENTAL TOFAUTI NI KWAMBA HAO MAPROFESA WALIKUFUNDISHA!
Report hii ya Lembeli haina jipya. Mambo aliyoyasema ndo yanaendelea kila siku hapa nchini. Yaani ni business as usual
ReplyDelete