
Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu A.O. Chitanda, huku pia waandishi
wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;
Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama,
Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, mjadala wake kwa upande wa chama
umeshafungwa, huku taratibu za kikatiba za ndani ya chama zikiendelea.
Pili suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa
taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya;
*1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
*2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).*
*3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
*4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
*5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.
Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake
ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter
Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.
Kupata taarifa kamili BOFYA HAPA


restructuring towawrds Movement For Christianity
ReplyDeleteondokeni mtuachie chama chetu cha kanisani, kwani hamkujua toka mwanzo tulikuwa tunawatumia tu kufikisha agenda zetu?
ReplyDeleteWAKATAFUTE NCHI YENYE 100% WATU WA ITIKADI YAO YA KIIMANI WAKAGOMBEE HUKO. SIYO BONGO
ReplyDeleteCHADEMA ni chama chetu sisi wa Kilimanjaro tu nyie wengine hatuwataki tutawaondoa tu polepole. Thubutu kamwe hatutaruhusu mtu kutoka mkoa mwingine kupata nafasi hasa ya mwenyekiti na halafu kugombea uraisi kama si kutoka Kilimanjaro. Hiyo ieleweke wazi kuwa ndiyo sera yetu.
ReplyDeletewewe anon wa nne hapo juu unaedai chadema ni chama chenu wakilimanjaro.,ninachoweza sema ni kuwa pole sana na ndani ya akili yako hakuna what so called AKILI,BUSARA. punguani kama wewe unahitaji msamaha na kuombewa ili Mwenyezi Mungu akusamehe.
ReplyDeleteSijui kwa nini ila hii habari ya "UDINI" nahisi kama inaudwa vile!!!
ReplyDeleteDhambi ya "UDINI" itamfuatilia mtu yule aliye iunda, itamganda kama ruba na mwishowe itamuangusha.