Kampuni ya Transevents Marketing Ltd ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious Transport(DAT) linalotengeneza mabasi  kutoka Uholanzi  yenye uwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayoanzia Tanzania.
Mabasi hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha swala zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.
Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu. Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu  kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.
Video hizi Mbili zinaelezea kwa kina na kuonesha jinsi Mabasi haya yatakavyokuwa yakifanya kazi hapa nchini Tanzania
Tazama Video za Basi hilo tangia Linatengenezwa hadi Linafanyiwa majaribio  
Tazama video ya Basi hilo Likiwa linafanya safari zake Nchi kavu na Baharini pamoja na abiria ndani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Haya mabasi bongo yatajaa mbuzi, kuku, ndizi, halafy yatazama kama mchezo vile, teknolojia inaenda sambamba na ustaarabu.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli mdau hapo juu. Also yanahitaji servicing ya kikweli sio za kijanjajanja karma bongo. Uingereza kuna moja ilishika moto siku za karibuni, nafikiri wakasuspend kutafutia chanzo chair name solution

    ReplyDelete
  3. Bahari hii hi yetu ya Hindi! iliyojaa mawimbi makubwa na siyo kama mito ya Rhine/ Thames/ Volga huko ulaya.

    Si amini mabasi haya yanaweza kufanya safari hizi majini ktk bahari ya Hindi mbali ya hata mto Ruaha au Rufiji.

    ReplyDelete
  4. ni kweli kbsa mdau hapo juu nakuunga mkono nyumbani ustaraabu F the capacity of bus is 45 passengers but they will be overloaded up to 60 ppl plus luggage itakua maafa tu ya ajali..

    ReplyDelete
  5. MSITULETEE VIFO DEREVA ANATAKIWA ASIWE NA MATATIZO YA PROBLEMS.

    NANI ANAZIJUA HIZO HESABU ZA KUTEMBEZA KITU HICHO HAPO BONGO HAO MADEREVA WA DALADALA

    ReplyDelete
  6. Jamani. Hii teknolojia isitusahau sisi wa Pemba. Tutajitahidi kuwaacha hao kuku na mafenesi ilimradi na sisi tukumbukwe. Hawa wamekezaaji wasihofu suala la abiria, kama wataweka viwango vya nauli zilizo rafiki kwa watu wa kipato cha kawaida, basi watatusaidia sana.

    ReplyDelete
  7. Wewe mdau wa kwanze hebu jaribu kuwa mstaarabu na wewe.

    Mbona mabasi ya daladala hayana mbuzi wala kuku? Yaani umetudharau namna hiyo kwa kuwa wewe uko Ulaya au wapi sijui.

    ReplyDelete
  8. Hayako efficient kusafiri masafa marefu. Ni mazito kulinganisha na mabasi ya kawaida. Hayawezi "kukata" maji kwa hiyo hayana mwendo wa kasi.

    Stability yake ni ndogo kwenye mawimbi. Kumbuka hata Mv Skagit haikuwa inaruhusiwa huko kwao Marekani kusafiri kwenye bahari za wazi.

    Haya yatafaa kuchukua watalii accross Kigamboni tu, tena bahari iwe imetulia.

    ReplyDelete
  9. eBU WAONYESHENI WANA SIASA WETU MUONE WATAKAVYOTUMIA VIZURI FURSA HIYO KWA UFANISI ULIOPITILIZA.

    ReplyDelete
  10. Mabasi ya Njia za MAJI na NCHI KAVU:

    Kila kitu kinawezekana chini ya jua na kilakitu ni Mipango,

    Nawakakikishia hakuna litakalo haribika kwa kuwa TUTAWEKA KAMERA ZA CCTV NDANI YA VYOMBO HIVYO GJALI SANA NA VYAMATAWI YA JUU VYA USAFIRI!!!

    ILI YULE ATAKAYE HUJUMU ATARUSHWA LIVE TBC TAIFA HADI AIBU FAMILIA YAKE ITAMSHUHUDIA AKIFAYA UPUUZI NDANI YA BASI!

    ZAIDI YA HAPO TUTAWEKA SHERIA KALI SANA NA ADHABU KWA YEYOTE MPUUZI ATAKAYE PATIKANA!

    KAMA IMEWEZEKANA KUTEKELEZA MPANGO MGUMU KAMA HUO WA MABASI, KWELI ITASHINDIKANA KUWAKABA MAKOO WACHECHE MIONGONI MWETU WAJINGA?

    ReplyDelete
  11. Kwa Maendeleo haya ya Mabasi ya Hadhi ya juu kabisa ambayo yanatutoa kimaso maso Watanzania, huyo atakayekunya ndani ya basi atakiona cha mtema kuni!

    Tutamrusa bila huruma Live TBC-1 akiwa anashusha mzigo !!!

    ReplyDelete
  12. Mdau wa kwanza ameminya panapouma, na ukweli unauma mdau wa saba.

    ReplyDelete
  13. Watanzania tusiwe wepesi kuwa excited na kuruhusu kwa urahisi matumizi ya vitu km hivi ambavyo vinaweza kuweka maisha ya raia wetu hatarini.
    Hawa jamaa wanawafanya watanzania guinea pig, kwa kujua uthibidi wa viwango vyetu ni dhaifu vilevile kupitia corruption wanaweza waka dump kila kila kitu hapa.Tusipokee vitu hivi..watueleze ni nchi gani iliyoendelea inayotumia mabasi yanayo elea, tunafahamu kwa hakika USA, Canada, UK etc sarakasi hii ya bahari haipo.
    Tunaomba akina Mwakyembe waambie hao jamaa wayatumie hayo mabasi wenyewe kwenda Zanzibar na kurudi kwa mwaka mmoja then tufikirie km tutayahitaji.ninakuhakikishia hakuna mzungu ataingia humo ndani ...
    Wake up fellows. ..

    ReplyDelete
  14. Haya yatakuwa mazingaombwe.usafiri kutoka Mombasa mpaka Mtwara kwa basi baharini? Seriously?
    Solution ya foleni Dar haihitaji teknogia hii.baadhi ya solution ya foleni serikali imeanza kushughulikia of which na believe ni more viable ie
    -kujenga daraja la kigamboni
    -mabasi yaendayo kasi.DAT
    -treni ya Mwakyembe.kwa hili linahitaji uboresho kwakutandaza reli za kisasa na kununua vichwa vya trni vya kisasa pia.
    -kupanua barax2, kuongeza lanes.
    -kuboresha na kuanzisha feeder roads.
    -kuhamisha baadhi ya ofisi za serikali, makampuni njee ya city centre.

    ReplyDelete
  15. Mabasi haya ni mazuri na ya manufaa sana kwa Watanzania. Kama alivyosema mtoa maoni hapo juu, mabasi haya yasisafiri katika bahari kuu tutapoteza maisha. Mawimbi ya bahari kubwa yana nguvu sana, sidhani kama mabasi haya yanaweza kuhimili nguvu ya mawimbi hayo, basi litoke Mombasa hadi Mtwara. Haiwezekani. Mabasi haya yatafaa sana katika safari za Kigamboni na sehemu zingine za jiji la Dar es salaam na pia safari za Dar, Kilwa na Mafia hata kufika hadi Mtwara katika safari fupi fupi sio kutoka Mombasa hadi Mtwara. Labda Mombasa na Pemba na Pemba na Unguja.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  16. naona watu wamesahau ile meli iliyozama kule znz na kuuwa mamia ya watu, ilichukua masaa kadhaa kabla ya kuzama na bado tulishindwa kuwaokoa ndugu zetu , sikwambii hii ikizama ni kwa dakika tu , msitafute sababu za maafa bure kwanza tuimarishe huduma za uokoaji inapotokea ajali , tukiweza ndio tufikirie makubwa , haya tuwaachie wenyewe kwa sasa

    ReplyDelete
  17. Nitalia sana iwapo yatafanikiwa kuletwa na kutumika Tz,licha ya sababu za usalama zilizosemwa na wadau waliotangulia......mimi nasema kwa njia iliyopangwa kutumiwa usafiri huu haina shida kivile ya usafiri kiasi cha kubuni mbadala huu, hapa kuna kitu kimejificha.....ivi kwanini sisi tume watu wa kufanyiwa majaribio kila siku????ningependa wafanye utafiti ni nchi ngapi zinatumia njia hii kwa usafiri, na kwa umbali gani.Isije ikawa zinatumika kwa utalii tena kwa umbali wa mita 500 tu.

    ReplyDelete
  18. Msitake kutuua kama inzi jamani!! Mabasi ya barabarani pekee ni chinjachinja tosha!! Vyombo vya majini rekodi zake sio za kujivunia!! Kwa kuchanganya hizi njia mbili ambazo kwetu zote ni MOTO MKALI, si SUICIDE??

    ReplyDelete
  19. Wazungu husema you will Never progress without trying new things....ndo maana mkulima anayetumia jembe la mkono akiendelea kutumia jembe hilo pasipokubadilisha zana ya kilimo ataendelea kuwa masikini,lakini akipata power tiller,kipato kitaongezeka,nadhani kwa watu wanopita Mwai Kibaki Road watskubaliana nami kuwa ni mda muafaka wa kuamua kuacha magari yao kwenye reserved parking nakutumia shuttle hizo kwenda maofisini stress free,They would rather opt for this than using their private drives,wachangiaji wengine hapo juu tusiwe na mawazo rigid,hayo magari obvious yatakuwa yametestiwa kwa viwango vya juu kuliko mabasi yenu haya ya chasis za scania....napita tu

    ReplyDelete
  20. Wahenga husema you Cannot progress without trying new things!!!!hata Mkulima akiendelea kutumia jembe la mkono hatakaa andelee mbele mpaka atakopokuwa tayari kutumia Powetiller au Tractor,nasi pia inabidi tuachane na mawazo mgando kwa faida ya kizazi kijacho,nani alijua kutakuwa na flyovers?Rapid Bus Transport?ukiangalia hatuna Road Reserves za kutosha,wakati Mv registration per year increases yearly,Be positive,coz naami ni hayo Mabasi yamekuwa certified na IOS ukilinganisha na mabasi yenu yalioundwa na Chasis za Malori

    ReplyDelete
  21. Nafikiri inabidi tupate Maelekezo ya Engineers especially Marine Engineers,coz inasemekana haya Mabasi ndo usafiri mkuu Netherlands,na pia ndo yaliwekwla kuondoa matumizi ya feri huko visiwa vya Scotish,yametengenezwa kwenye Platform ya basi nakuwekewa Marine hull za Hamilton jets inayoliwezesha kuelea katika maji ya mkondo wowote...Afrika tubadilike na sisi,ckhiz kuna hata ndge za kwenda mikoani kwenu,zamani watu wamekuwa wakisafiri kwa Uongo...lol

    ReplyDelete
  22. Mimi naona wadau tuchangie hasa kwa kukudadisi ili tujue vizuri hasa yameundwa kwa technolojia gani,kwasababu hata bajaji hatukuwahi kuzijua, zamani tuliamini nikwaajiri ya ndugu zetu walemavu, kumbe siyo,naungana na baadhi ya wadau hapo juu japo nina wasiwasi kuwa Mabasi yaendayo kasi hasa lengo nikupunguza madaladala na uwingi wa watu barabarani, lakini siyo kukufanya wewe uliye na Rav4 ukaamua upande Treni,au Basi bado ninawasiwasi na hilo

    ReplyDelete
  23. Pia tukumbuke miaka 10 mpaka 20 ijayo idadi ya magari itakuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, watoto wetu kizazi hiki tumewalea kupenda sana magari, hivyo angalia hizo feeder roads zitafeed wapi? Kupanua barabara bado hatuna reserve ya kutosha, angalia foleni ya Obama Road kuja mpaka Bank M utabomoa nyumba yanani ili utanue barabara, ni vema nchi kama nchi ikaangalimia means nyingi za ku evacuate watu mjini kuelekea majumbani

    ReplyDelete
  24. Most land vehicles –can be made amphibious simply by providing them with a waterproof hull and perhaps a propeller. This is possible as a vehicle's displacement is usually greater than its weight, and thus will float. Heavy vehicles however sometimes have a density greater than water (their weight in kilograms exceeds their volume in litres), and will need additional buoyancy measures. These can take the form of inflatable floatation devices, much like the sides of a rubber dinghy, or a waterproof fabric skirt raised from the top perimeter of the vehicle

    ReplyDelete
  25. Amphibious Bus Has been a proven performer with successful operations in 16 countries around the world including: Bermuda, Dubai, England, Ireland, Japan, Malaysia, Puerto Rico, Virgin Islands, Alaska, Boston, California, Florida, Hawaii, New York, and Rhode Island. The design is fully patented and UNSINKABLE; even with the drain plugs removed and the full engine room flooded!One of the Commenter above wanted to know if his Benchmark countries,USA, CANADA and UK have tried this technology

    ReplyDelete
  26. Mchango wangu kwa leo hapo nikuwa Pengine hili tuchukulie kama changamoto kwa Mamlaka na Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zinazojihusisha na maswala ya usafirishaji pengine wa majini na nchi kavu waangalie ni namna gani hili linawezekana au haliwezekani,kwasababu kwa kuangalia mm naona kwanza kuna "Ocean Tourism Attraction" wageni wanatoka zao Serena Hotel, holiday inn, Kempesky hao mpaka Bagamoyo au mpaka Saadan, je nchi haijapata chenji hapo?fungukeni jamani..

    ReplyDelete
  27. 1.National Institute of Transport ????
    2.Sumatra
    3.Commissioner of TRA
    4.Commissioner of Insurance
    5.Ministry of Transport
    6.Ministry of Infrastracture
    7.Ministry of home affairs_Coast Guard
    8.Ministry of Tourism....
    Changamoto kwenu...fursa hiyo wenzenu wanajenga reli kutoka Mombasa mpaka Rwanda angalieni watu wanvyopata shida visiwa vya mafia huko na kwingineko kote along the coast

    ReplyDelete
  28. Kama nayaona Mahotel ya zanzibar kando kando ya bahari yakigombea mabasi hayo...siyo siri hiyo kwel Ocean Tourism....nawasihi wenye mahotel ufukweni tuleteeni raha nyingine wateja wenu bana...Tehe!!

    ReplyDelete
  29. Technical Specification For The Amphibious Buses: HAVE A LOOK AND COMMENT AGAINST THE ORDINARY DOMESTIC BUSES WE ARE USING...OR call me..+255 768 220 555 or +255 659 233 311 for Clarification.

    Technical Specifications
    Comfort: Kiel seating Water drive Electrical driven Water safety Watertight compartments
    Toilet Block Voith air type VIP380 50 life jackets
    50kW 5 emergency exits
    Capacities 50 passengers Manoeuvring Bowtruster 10kW
    ( including driver & deckhand) Sterntruster 7.5kW Colour RAL colours
    Batteries 190 Lithium ion
    Technical Specifications Volvo engine
    Vehicle dimensions Length 14.02metres
    Width 2.55metres
    Height 3.22metres
    Wheelbase 6.8metres
    Empty weight 21000kg
    Draft when floating 1.8 metres Certification Class3 city bus
    Dutch Marine Certification


    Peformance Max Roadspeed : 80km/h
    Max speed at sea: 3 knots Options Airco system
    Entertainment system
    Panoramic roofwindows Builder Dutch Amphibious Transport Vehicles/J.de Jong Scheepsservice
    Nijmegen, The Netherlands
    Propulsion Rear wheel drive Options Airco
    Air suspension Entertainment system
    Automatic limited slip differential Road safety Electric fly drive
    Body cage roll over tested, ABS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...