Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika Eneo la Maziwa Makuu, Mary Robinson akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, baada ya yeye na Bw. Martin Kobler (kulia) ambaye ni Muwakilishi wa Katibu Mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa MONUSCO kuwasilisha taarifa zao mbele ya Baraza Kuu la Usalama, katika mkutano wa ndani wa Baraza hilo uliofanyika siku ya jumatano. katika mkutano huo wakuu hao wawili walielezea kuridhishwa kwao na hali ya kijeshi na kisiasa inavyoendelea katika DRC hususani eneo la Mashariki ya nchi hiyo. pamoja na mchakato wa utekelezaji wa Mpango Mpana wa Umoja wa Mataifa kuhusu siasa, amani, usalama na maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa na matarajio kuhusu mazungumzo ya Kampala ( Kampala Talks).
Home
Unlabelled
TUMEWADHIBITI M23 NGUVU ZETU SASA ZIKO KWA FDLR- MONUSCO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...